Watatu wauawa na kisha miili yao kutupwa msituni

Miili ya watu watatu ambao ni waendesha pikipiki maarufu bodaboda imeokotwa katika msitu ya Kijiji cha Hiari wilaya ya Mtwara mkoani Mtwara.

0

Miili ya watu watatu ambao ni waendesha pikipiki maarufu bodaboda imeokotwa katika msitu ya Kijiji cha Hiari wilaya ya Mtwara mkoani Mtwara.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Nicodemus Katembo amesema kuwa tukio la kwanza limetokea katika Kijiji cha Hiati ambapo viliokotwa viungo vinavyodhaniwa kuwa vya binadamu ambavyo ni mifupa, ugoko na utumbo mdogo.

Amesema viungo hivyo vinadhaniwa kuwa ni vya mwendesha bodaboda, Kelvin Mbale ambaye alitoweka tangu Februari 2, 2022.

Kamanda Katembo amesema katika eneo la tukio zilipatikana nguo na viatu ambapo ndugu walivitambua kuwa vilikuwa vya marehemu.

Kamanda huyo amesema kuwa katika tukio la pili linahusisha mauaji ya Mohamed Juma ambaye anadaiwa kuuawa na watu wasiojulikana kwa kuchomwa kitu chenye ncha kali

 Amesema kuwa tukio hilo limetokea Februari 12, 2022 maeneo ya pori la Majengo Wilaya ya Mtwara.

Amesema kuwa taarifa zinaonyesha kuwa Juma alipakia watu wawili wakiwa na mabegi mgongoni na kuelekea kusikojulikana na baadaye bodaboda wenzake walianza kumtafuta maeneo kukukuta mwili wake katika pori hilo.

Mwili huo umepelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara ya Ligula kwa ajili ya kuhifadhiwa huku ukisubiri ndugu wa marehemu kwa ajili ya uchunguzi.

Katembo amesema Februari 15, 2002 Polisi walipokea taarifa ya kupatikana kwa mwili mwendesha bodaboda, Mohamed Juma Mohamed (22).

Amesema upelezi wa matukio hayo unaendelea kuwabaini wote waliohusika na mauaji hayo.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted