Watu wanane wafariki katika moto Ivory Coast

Watu wanane walifariki na wengine kadhaa kujeruhiwa wakati moto ulipoteketeza duka la kuoka mikate magharibi mwa Ivory Coast siku ya Jumatano, mamlaka ya eneo hilo ilisema. Moto huo...

0

Watu wanane walifariki na wengine kadhaa kujeruhiwa wakati moto ulipoteketeza duka la kuoka mikate magharibi mwa Ivory Coast siku ya Jumatano, mamlaka ya eneo hilo ilisema.

Moto huo ulizuka asubuhi katika duka la Man, mojawapo ya miji mikuu katika taifa hilo la Afrika Magharibi, ofisi ya meya ilisema.

“Kumekuwa na uharibifu mkubwa wa nyenzo, majeraha makubwa na, kwa bahati mbaya,  watu wanane wamefariki, meya wa jiji hilo alisema katika taarifa.

“Watu wanaomboleza,” naibu wa eneo hilo Sidiki Konate alisema kwenye Facebook, na kuongeza kuwa moto huo ulisambaa kutoka kwa duka la kuoka mikate hadi majengo mengine katika kitongoji hicho.

Alichapisha video fupi ya moto huo kwenye Facebook, zima moto walifaulu kuuzima moto huo baadae asubuhi hiyo.

Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted