Misri yaapa kuwatunza Warusi na wa Ukraine waliokwama nchini humo

Uamuzi huo ulifuatia msururu wa kufutuliwa mbali kwa safari za ndege baada ya Urusi kupeleka wanajeshi wake nchini Ukraine.

0
Mji wa kitalii wa Sharm el Sheikh

Misri ilisema Alhamisi itawashughulikia watalii wowote wa Urusi na Ukraine waliokwama nchini humo kwa sababu ya safari za ndege kufutiliwa mbali kutokana na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Watalii kutoka nchi ambako usafiri wa anga umetatizwa wataweza ‘kusalia katika hoteli waliko nchini Misri hadi watakaporejea nyumbani salama,’ wizara ya utalii ilisema.

Uamuzi huo ulifuatia msururu wa kufutuliwa mbali kwa safari za ndege baada ya Urusi mapema Alhamisi kupeleka wanajeshi wake nchini Ukraine.

Safari za ndege kutoka kwa viwanja 11 vya ndege kusini mwa Urusi na uwanja mmoja wa ndege huko Crimea inayokaliwa na Moscow zimeghairiwa, mamlaka kuu ya usafiri wa anga nchini Urusi imesema.

Shirika la ndege la Ufaransa Air France na shirika la ndege la Ujerumani Lufthansa pia wamesitisha safari za ndege kuelekea Ukraine.

Wakati mataifa ya Magharibi yametangaza vikwazo vipya vikali dhidi ya Urusi, wizara ya mambo ya nje ya Misri siku ya Alhamisi ilitoa wito wa ‘mazungumzo na suluhisho ya kidiplomasia’ ili kuepusha maafa zaidi.

Hoteli zote kwenye pwani ya Red Sea nchini Misri ni maarufu kwa watalii wa Ukrainia na Warusi.

Utalii unawakilisha takriban asilimia 10 ya Pato la Taifa la Misri, ambapo theluthi moja ya wakazi milioni 100 wanaishi kwenye umaskini.

Sekta hiyo imeathiriwa mara kwa mara katika muongo mmoja uliopita, na machafuko yaliyohusishwa na uasi wa 2011, mashambulizi ya jihadi na vikwazo vya usafiri juu ya janga la UVIKO19.

Safari za ndege za moja kwa moja kutoka Urusi hadi mji wa Sharm el-Sheikh zilianza tena mwaka jana, kufuatia marufuku ya Urusi ya kutungua ndege iliyoua 224 wengi wao wakiwa Warusi mnamo 2015.

Kundi la Islamic State lilidai kutekelza shambulizi hilo.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted