KENYA: Mwanafunzi ahukumiwa jela miaka mitano kwa kosa la kuua bila kukusudia

Msichana mmoja raia wa Kenya amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kwa kosa la kuua bila kukusudia kufuatia kuchoma moto katika bweni la shule na kuua wenzake tisa.

0

Msichana mmoja raia wa Kenya amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kwa kosa la kuua bila kukusudia kufuatia kuchoma moto katika bweni la shule na kuua wenzake tisa.

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 18 alitenda kosa hilo mwaka wa 2017 akiwa na umri wa miaka 14 katika mwaka wake wa kwanza wa shule ya upili katika Shule ya Wasichana ya Moi katika mji mkuu, Nairobi.

Mahakama ilikuwa imefahamishwa kwamba alijaribu kujitoa uhai mara mbili kabla ya kuwasha moto ndani ya chumba chake cha malazi.

Wazazi na walezi wa wanafunzi waliofariki kwenye moto huo wanasema hukumu hiyo ni ndogo lakini wanafurahi kwamba haki imetendeka, kulingana na ripoti katika vyombo vya habari vya nchini humo.

Visa vya uchomaji moto vimekuwa tatizo la kawaida katika shule za bweni nchini Kenya katika miongo miwili iliyopita.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted