Afrika Kusini haijarekodi vifo vyovyote vinavyotokana na UVIKO 19, kwa mara ya kwanza tangu Mei 2020

Afrika Kusini iliripoti karibu vifo 100,000 vilivyotokana na UVIKO 19, na zaidi ya kesi milioni 3.6 za maambukizi.

0

Afrika Kusini haijaripoti vifo vyovyote vinavyotokana na UVIKO-19 katika siku mbili zilizopita, kwa mara ya kwanza tangu Mei 2020, mamlaka ya afya ilisema Jumanne.

UVIKO 19 iliiathiri Afrika Kusini zaidi kuliko nchi nyingine yoyote barani Afrika, habari kuwa idadi ya vifo imepungua imekuwa habari njema kwa nchi hiyo.

Taasisi ya Kitaifa ya Magonjwa ya Kuambukiza ilitoa tangazo hilo katika hesabu yake ya kila siku ya kesi za UVIKO 19, na hivyo kuzua matumaini  miongoni mwa viongozi wa afya.

Mara ya mwisho kwa nchi hiyo kuripoti kuwa hakuna vifo kwa muda wa saa 48 ilikuwa Mei 12, 2020.

“Kwa hakika, hospitali hazina wagonjwa wa UVIKO-19,” alisema Shabir Madhi, profesa wa chanjo katika Chuo Kikuu cha Witwatersrand.

“Tunajua kwamba vifo vilivyoripotiwa ni chini ya takriban tatu, lakini hata hivyo kiwango kwa sasa ni cha chini sana.”

Alisema kupungua kwa vifo kunatokana na utoaji wa chanjo na athari za mawimbi ya maambukizo yaliyopita.

Hali hii imekuja kwa gharama kubwa ya watu kupoteza maisha, lakini imesababisha sehemu kubwa ya idadi ya watu ambao kwa sasa wamepata kinga dhidi ya ugonjwa huo.”Madhi alisema.

Takriban asilimia 80 ya jimbo lenye watu wengi la Gauteng tayari limeambukizwa Covid, takwimu ambayo aliamini kuwa inaweza kuakisi nchi nzima.

Zimbabwe, Namibia, Angola, Msumbiji na Eswatini pia ziliripoti hakuna vifo vinavyotokana na UVIKO 19 katika saa 24 iliyopita, ingawa nchi hizo jirani zina mfumo hafifu wa ufuatiliaji wa masuala ya afya.

Afrika Kusini iliripoti karibu vifo 100,000 vilivyotokana na UVIKO 19, na zaidi ya kesi milioni 3.6 za maambukizi.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted