Moderna yaanzisha kituo cha kwanza cha kuzalisha chanjo ya UVIKO 19 nchini Kenya

Moderna ilisema ilitarajia kuwekeza dola milioni 500 katika kituo hicho kipya, ambacho kitatoa chanjo kwa bara la watu bilioni 1.3.

0

Watengenezaji chanjo nchini Amerika, Moderna walitangaza Jumatatu kwamba watajenga kituo chake cha kwanza cha kuzalisha chanjo ya mRNA barani Afrika baada ya kutia saini makubaliano na serikali ya Kenya kuzalisha hadi dozi milioni 500 kwa mwaka.

Kampuni hiyo ilisema ilitarajia kuwekeza dola milioni 500 (euro milioni 460) katika kituo hicho kipya, ambacho kitatoa chanjo kwa bara la watu bilioni 1.3.

“Kupambana na janga la UVIKO-19 katika miaka miwili iliyopita kumetoa ukumbusho wa kazi ambayo lazima ifanywe ili kuhakikisha usawa wa afya duniani. Moderna imejitolea kuwa sehemu ya suluhisho,” Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Stephane Bancel alisema katika taarifa.

Moderna alisema inatarajia kutumia kituo hicho kusambaza dozi za ugonjwa wa UVIKO-19 kwa mataifa ya Afrika mapema mwaka ujao, katika nia ya kuongeza chanjo katika bara hilo lenye idadi ndogo ya watu waliochanjwa duniani.

“Uwekezaji wa Moderna nchini Kenya utasaidia kuendeleza upatikanaji sawa wa chanjo duniani kote na ni ishara ya maendeleo ya kimuundo ambayo itawezesha Afrika kuwa kiungo muhimu ya ukuaji endelevu wa kimataifa,” Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alisema.

Zaidi ya mwaka mmoja baada ya chanjo ya kwanza dhidi ya UVIKO 19 kupeanwa, ni asilimia 12.7 tu ya Waafrika wamechanjwa kikamilifu, kulingana na Vituo vya Afrika vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC).

Janga hili limefichua utegemezi mkubwa wa Afrika kwa chanjo zinazoagizwa kutoka nje na udhaifu wake wa kiufundi ikilinganishwa na Ulaya, China na Amerika.

Tangazo la Moderna linafuatia uamuzi wa Shirika la Afya Ulimwenguni kuunda kitovu cha chanjo ya kimataifa ya mRNA nchini Afrika Kusini mwaka jana, huku Kenya ikiwa miongoni mwa mataifa sita ya Afrika yaliyochaguliwa kuwa wapokeaji wa kwanza wa teknolojia inayolenga kuwawezesha wazalishaji chanjo nchini Kenya kuzalisha chanjo hiyo.

Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amerudia wito wa kupatikana kwa chanjo kwa usawa ili kukabiliana na janga hili, na kushambulia mataifa Tajiri kwa kujiimbikizia chanjo.

Hivi sasa ni asilimia moja tu ya chanjo zinazotumiwa barani Afrika zinazozalishwa barani humo.

Ulaya — makazi ya baadhi ya makampuni makubwa yaliyobuni chanjo hiyo – yamepinga hatua hiyo, ikisema kwamba kipaumbele cha kwanza kilikuwa kujenga uwezo wa uzalishaji katika nchi maskini zaidi.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted