Watu wanne wafariki kutokana na homa ya manjano nchini Kenya

Ugonjwa huo huenezwa na mbu wale wale wanaoneza magonjwa ya Zika na dengue.

0

Mlipuko wa homa ya manjano, ugonjwa hatari na unaoambukiza, umesababisha vifo vya watu wanne nchini Kenya tangu ulipogunduliwa kwa mara ya kwanza Januari, wizara ya afya ilisema Jumatatu.

Visa hivyo viliripotiwa katika kaunti ya Isiolo, takriban kilomita 270 kaskazini mwa mji mkuu Nairobi.

Watu wanne wamefariki kutokana na ugonjwa huo,” Patrick Amoth, mkurugenzi mkuu wa wizara ya afya ya Kenya, alisema.

Hakuna matibabu mahususi ya homa ya manjano, ugonjwa wa kuvuja damu unaoenezwa na mbu walioambukizwa na unaopatikana katika sehemu za Afrika na eneo la Amazoni la Amerika Kusini.

Ugonjwa huo huenezwa na mbu wale wale wanaoneza magonjwa ya Zika na dengue.

Kenya, ambayo haijakumbwa na mlipuko wa homa ya manjano tangu miaka ya 1990, iligundua kisa chake cha kwanza katika miongo kadhaa Januari 12 na hadi wiki jana iliwatenga wagonjwa 15 waliokuwa na homa na maumivu ya misuli.

Hatari ya kuenea zaidi ilikuwa ndogo kwani mlipuko huo ulikuwa katika eneo lenye watu wachache, Amoth alisema.

“Kwa sababu ya idadi ndogo ya watu Isiolo, na jinsi watu wanakaa mbali mbali, inafanya kuwa rahisi kudhibiti,” Amoth alisema.

Mlipuko huo unaongeza changamoto za kiafya nchini Kenya huku Kenya ikiendelea kukabiliana na janga la UVIKO-19 na kupambana na ukame mkali huko Isiolo na kaunti zingine za kaskazini.

Ugonjwa huo huambukizwa kutoka kwa binadamu kwenda kwa binadamu kupitia mbu.

Chanjo za homa ya manjano hupendekezwa mara kwa mara kwa wasafiri wanaosafiri nchini Kenya.

Vyandarau, dawa za kuzuia wadudu pia huchukuliwa kuwa aina nzuri ya kujilinda na umbu wanaosababisha ugonjwa huo.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted