Heineken, Universal Music kati ya kampuni za hivi punde kuondoka Urusi

Kampuni nyingine McDonald’s, Coca-Cola na Starbucks waliondoa biashara zao Urusi

0
Kampuni ya bia ya Heineken Astrid Stawiarz/Getty Images for NYCWFF/AFP (Photo by Astrid Stawiarz / GETTY IMAGES NORTH AMERICA / Getty Images via AFP)

Kampuni ya kutengeneza bia ya Uholanzi Heineken na Universal Music Group zimekuwa kampuni za hivi punde zaidi za Magharibi kusimamisha shughuli zake nchini Urusi kutokana na vita vya Urusi nchini Ukraine.

Kampuni hiyo ya pili kwa ukubwa duniani ya bia ilisema Jumatano ilikuwa inasimamisha uzalishaji, utangazaji na uuzaji wa chapa ya Heineken nchini Urusi “ili kukabiliana na kuendelea kwa vita.”

Heineken tayari ilikuwa imesimamisha uwekezaji mpya na mauzo yake nchini Urusi wiki iliyopita.

“Tumeshtushwa na kuhuzunishwa kuona mkasa huo ukiendelea nchini Ukraine,” afisa mkuu mtendaji wa Heineken Dolf van den Brink alisema katika taarifa yake.

Vita vya serikali ya Urusi dhidi ya Ukraine ni shambulio lisilochochewa na lisilostahili kabisa,” alisema.

Heineken imeajiri watu 1,800 nchini Urusi na inasema ni kampuni ya tatu kwa ukubwa nchini humo, ambapo inatengeneza chapa za Zhigulevskoe na Oxota kwa soko la nchini humo.

“Heineken haitakubali tena faida yoyote ya kifedha inayotokana na biashara zetu nchini Urusi,” ilisema.

Chapa nyingine maarufu za Heineken ni pamoja na Amstel, Tiger na Strongbow cider.

Takriban makampuni 300 yametangaza kujiondoa nchini Urusi tangu ilipovamia nchi jirani ya Ukraine, kulingana na watafiti wa Chuo Kikuu cha Yale.

Kampuni nyingine McDonald’s, Coca-Cola na Starbucks waliondoa biashara zao nchini Urusi.

Watu wakila katrika mgahawa wa McDonald’s mjini Moscow mnamo March 9, 2022. (Photo by AFP)

Siku ya Jumanne, Universal Music Group, kampuni kubwa zaidi duniani ya muziki, ilisema inasitisha shughuli zake zote na kufunga ofisi zake nchini Urusi mara moja.

“Tunahimiza kukomeshwa kwa ghasia nchini Ukraine haraka iwezekanavyo,” Universal ilisema katika taarifa yake.

“Tunazingatia vikwazo vya kimataifa na, pamoja na wafanyakazi wetu na wasanii, tumekuwa tukifanya kazi na makundi kutoka mataifa mbalimbali … kusaidia juhudi za misaada ya kibinadamu kuleta msaada wa haraka kwa wakimbizi katika kanda,”ilisema.

Kwingineko, kampuni kubwa ya reli ya Ufaransa ya Alstom ilitangaza Jumatano kuwa inasitisha usafirishaji kwa Urusi pamoja na uwekezaji wa biashara wa siku zijazo nchini humo.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted