Mwandamanaji aliyeoneka kwenye runinga ya Urusi huenda akahukumiwa kifungo cha miaka 15 gerezani

Mwezi huu Urusi ilipitisha vifungo vya sheria vya kifungo cha hadi miaka 15 jela kwa kueneza habari za uwongo zenye lengo la kudhalilisha jeshi lake, pamoja na kifungo...

0
Mwanamke aliyepinga vita vya Urusi nchi Ukraine aonekana nyuma ya mtangazaji Yekaterina Andreyeva wa kituo cha Urusi cha Channel One. Mwanamke huyo Marina Ovsyannikova ambaye pia ni mhariri katika kituo hicho, aonekana na bango la kutaka kusitishwa kwa vita. (Photo by AFP)

Mwanamke ambaye alipinga vita vya Urusi nchini Ukraine wakati wa habari katika kituo cha TV ya serikali huenda akahukumiwa kifungo cha miaka 15 jela, wakili wake alisema Jumanne.

Marina Ovsyannikova, aliingia kwenye chumba cha matangazo ya habari za jioni yanayotazamwa zaidi nchini Urusi kwenye Channel One Jumatatu jioni, akiwa ameshikilia bango linalosomeka “Tumalize Vita.”

Lilikuwa tukio lisilo la kawaida nchini Urusi ambapo vyombo vya habari vya serikali vinadhibitiwa vikali.

“Natarajia mteja wangu, Marina Ovsyannikova, atakabiliwa na si shtaka la kiutawala bali la jinai chini ya sheria mpya ambayo ina adhabu ya hadi miaka 15 jela,” wakili Daniil Berman aliiambia AFP.

Mwezi huu Urusi ilipitisha vifungo vya sheria vya kifungo cha hadi miaka 15 jela kwa kueneza habari za uwongo zenye lengo la kudhalilisha jeshi lake, pamoja na kifungo cha hadi miaka mitatu jela kwa kuitisha vikwazo dhidi ya Urusi.

Ovsyannikova, mhariri katika kituo hicho, alizuiliwa haraka baada ya tukio hilo.

“Kuna uwezekano mkubwa kuwa mamlaka itatumia kisa hicho kama mfano ili kuwanyamazisha waandamanaji wengine,” Berman aliongeza.

“Bado sijaweza kukutana na mteja wangu au kuthibitisha mahali anazuiliwa,” aliongeza, akilalamika kuhusu “tabia isiyo halali lakini ya kawaida” ya kuwanyima watu waliozuiliwa kuwasiliana na wakili wao.

Aliongeza kuwa mteja wake ana watoto wawili wadogo chini ya umri wa miaka 14.

Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov aliita tukio hilo “kitendo cha uhuni” lakini ukurasa wa Ovsyannikova wa Facebook umevutia zaidi ya ‘likes’ 100,000.

Channel One ilisema uchunguzi wa ndani unaendelea.

Tukio hilo lilipeperushwa sana na vyombo vya habari vya kimataifa na Urusi, ambavyo vilififisha ujumbe kwenye bango hilo ili kuepuka kukiuka sheria mpya ya vyombo vya habari.

Bango lililoandikwa kwa mkono lilisema ”Komesha Vita” kwa Kiingereza.

Hapo chini, ilisoma kwa Kirusi: “Acha vita. Usiamini propaganda. Wanakudanganya hapa.”

Bango lilikuwa limesainiwa kwa Kiingereza: “Warusi wanaopinga vita.”

Ovsyannikova aliweza kusema maneno machache kwa Kirusi, ikiwa ni pamoja na “Acha vita!” Wakati mtangazaji Yekaterina Andreyeva alipojaribu kumtoa nje kwa kuzungumza kwa sauti kubwa kabla ya kituo kisha kuweka kwa haraka picha za hospitali.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted