Mtoto wa miaka 14 adaiwa kuwalawiti watoto wenzie 19.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani humo, Allan Bukumbi ni kwamba Mtoto huyo anadaiwa kutumia pipi na biskuti kama njia ya kuwalaghai wenzake ili akamilishe adhma yake...

0

Polisi mkoani Iringa nchini Tanzania inamshikilia mtoto mwenye umri wa miaka 14 kwa tuhuma za kuwalawiti watoto wenzake 19.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani humo, Allan Bukumbi ni kwamba Mtoto huyo anadaiwa kutumia pipi na biskuti kama njia ya kuwalaghai wenzake ili akamilishe adhma yake ya kuwalawiti.

Kamanda Bukumbi amesema mtoto huyo amekamatwa baada ya ofisa Mtendaji wa Kata ya Kihesa Kilolo, Elizabeth Lugenge kutoa taarifa ya kuwepo kwa watoto watatu wanaosoma katika shule ya Msingi Igeleke kulawitiwa.

Amesema baada ya mahojiano, watoto hao walikubali na kuwataja wenzao watano.

“Na hao watano walipohojiwa wakawataja wengine watano hivyo kufanya idadi ya watoto 13. Mtuhumiwa alipohojiwa alikubali na akawatraja watoto wengine sita, wakawa 19,” amesema Bukumbi.

Amesema mtuhumiwa amesema alikuwa akichukuwa fedha kwa bibi yake, ananunua pipi kama mbinu ya kuwapata wenzake ili awafanyie kitendo hicho.

“Kwa hiyo watoto walipokuwa wanaenda kuangalia TV aliwagawia pipi na biskuti kama njia ya kuwalaghai,” amesema.

Ameeleza kuwa watoto wote waliotajwa walipelekwa katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa na Frelimo na uchunguzi ukabaini kuwa wamelawitiwa.

Aidha amesema upelelezi umekamilika huku kesi nane zikiwa zimefunguliwa ambapo watoto hao walilawitiwa kwa nyakati tofauti, hivyo mtuhumiwa atapelekwa mahakamani

“Fikiria hili tukio sio la mara moja, hawa watoto walikuwa wakifanyiwa mara kwa mara lakini wazazi hawakujua, ila mtendaji wa kata alipata taarifa shuleni. Tunakwama wapi wazazi na walezi? Hili ni tatizo,” amesema Bukumbi.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted