Mwezi mmoja wa vita vya Ukraine na Urusi, mamia ya watu wafariki wengine wakimbia  makazi yao.

Leo Machi 24, Ukraine inatimiza mwezi mmoja tangu iingie kwenye vita na Urusi baada ya Urusi kuanza kuishambulia Ukraine Februari 24.

0

Leo Machi 24, Ukraine inatimiza mwezi mmoja tangu iingie kwenye vita na Urusi baada ya Urusi kuanza kuishambulia Ukraine Februari 24.

Hadi sasa zaidi ya raia milioni moja nchini Ukraine wameyakimbia makazi yao kufuatia vita hivyo ambavyo bado vinaendelea kuitesa nchi hiyo na raia wake.

Urusi imekataa kuweka silaha zake chini ili kusitisha vita hiyo ambayo ndiye mwanzilishi licha ya kuwa wito kutolewa kwa Rais wa Urusi, Vladmir Putin kusitisha vita hivyo na badala yake yawepo mazungumzo ya upatanishi kati yake na Ukraine.

Jana Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, ametoa wito kwa watu duniani kote kuandamana barabarani kama hatua ya kupinga uvamizi wa Urusi nchini Ukraine. 

Katika ujumbe alioutoa kuhusu  kumbukumbu ya mwezi mmoja wa uvamizi wa Urusi, Zelensky amewataka watu duniani kote kusimama imara dhidi ya Urusi na kupinga vita hivyo. 

Rais huyo wa Ukraine pia ametoa wito kwa muungano wa jeshi la kujihami la NATO, kuipa msaada Ukraine ikiwemo wa silaha ili kupambana na wanajeshi wa Urusi. 

Mamia ya watu wameuawa, na mamia ya wengine wamejeruhiwa huku zaidi ya raia milioni 3 wa Ukraine wakiimbia nchi yao na kutafuta hifadhi katika mataifa jirani. 

Urusi iliivamia jirani yake Ukraine mnamo Februari 24 kwa lengo la kuizuia nchi hiyo kuelekea Umoja wa Ulaya na kujiunga na NATO.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted