WHO: Zaidi ya theluthi mbili ya Waafrika waliambukizwa UVIKO 19

Wakati janga hilo limekuwa na athari mbaya kwa sehemu zingine za ulimwengu, Afrika ilionekana kuepuka athari hizo na haikuathiriwa vibaya kama ilivyohofiwa mwanzoni mwa janga hilo.

0

Zaidi ya theluthi mbili ya Waafrika wanaweza kuwa wameambukizwa UVIKO-19 katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, karibu mara 97 zaidi ya maambukizi yaliyoripotiwa, ripoti ya Shirika la Afya Ulimwenguni ilisema Alhamisi.

Vipimo vya kimaabara vimegundua visa milioni 11.5 vya Covid na vifo 252,000 katika bara zima la Afrika.

Lakini WHO kanda ya Afrika ilisema utafiti wake — ambao bado unakaguliwa — unapendekeza kuwa idadi iliyothibitishwa rasmi “inawezekana tu ilikuwa kiwango kidogo ya  kiwango halisi cha maambukizi ya coronavirus barani Afrika.”

“Uchambuzi mpya wa meta wa uchunguzi wa kiwango cha maambukizi ya sero-uenezi umebaini kuwa idadi halisi ya maambukizo inaweza kuwa mara 97 zaidi ya idadi ya kesi zilizothibitishwa,”alisema mkuu wa WHO Afrika Matshidiso Moeti.

“Hii inaonyesha kuwa zaidi ya theluthi mbili ya Waafrika wote wameambukizwa virusi vya UVIKO-19,” aliongeza.

Ripoti hiyo ilichambua zaidi ya tafiti 150 zilizochapishwa kati ya Januari 2020 na Desemba mwaka jana.

Ilionyesha mfiduo wa virusi uliruka kutoka asilimia tatu tu Juni 2020 hadi asilimia 65 kufikia Septemba mwaka jana.

“Kwa hali halisi, hii inamaanisha kuwa mnamo Septemba 2021, badala ya kesi milioni 8.2 zilizoripotiwa, kulikuwa na milioni 800,” Moeti alisema.

Wastani wa kimataifa wa idadi ya maambukizi ya kweli ni mara 16 zaidi ya idadi ya kesi zilizothibitishwa.

Huku kukiwa na uhaba wa vifaa vya kupima kwa idadi kubwa ya watu wa Afrika, maambukizo mengi hayakutambuliwa, kwani upimaji ulikuwa kwa wagonjwa wenye dalili hospitalini na wasafiri waliohitaji matokeo ya PCR.

“Lengo lilikuwa sana katika kupima watu ambao walikuwa na dalili wakati kulikuwa na changamoto katika upatikanaji wa vifaa vya kupima.”na hii ilisababisha “kurekodiwa kwa idadi isiyo halisi ya watu ambao wameambukizwa,” alisema Moeti.

Hofu ya mlipuko imeonekana kuwa mbaya

Moeti alisema kutoa data sahihi katika bara hilo, ambalo kwa kiasi kikubwa lina vituo vya afya duni na visivyo na rasilimali, imekuwa vigumu kwa sababu “asilimia 67” ya watu katika bara hilo hawaonyeshi dalili zozote.

Wakati janga hilo limekuwa na athari mbaya kwa sehemu zingine za ulimwengu, Afrika ilionekana kuepuka athari hizo na haikuathiriwa vibaya kama ilivyohofiwa mwanzoni mwa janga hilo.

Kuwepo kwa vituo vya afya na huduma dhaifu, wataalam wengi walikuwa na hofu kwamba mifumo hiyo itazidiwa.

Uchambuzi kadhaa umefanywa wa muundo wa janga hilo barani Afrika, na wengine wakihitimisha kuwa idadi kubwa ya vijana barabi humo ilifanya kama kinga dhidi ya ugonjwa huyo.

Nchini Ghana, utafiti wa WHO ulionyesha kwamba walioambukizwa zaidi walikuwa vijana, kulingana na Dk Irene Owusu Donkor wa Taasisi ya Noguchi Memorial ya Utafiti wa Kimatibabu.

Nchi nyingi za Kiafrika zimezoea milipuko ya magonjwa.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted