Kenya: Google kuanzisha kituo cha kwanza kikubwa Afrika, jijini Nairobi

Google ni kati ya makampuni makubwa ya kiteknolojia yanayoanzisha vituo vya uvumbuzi jijini Nairobi.

0

Kampuni ya teknolojia ya kimataifa ya Amerika,Google imetangaza kuwa itaanzisha kituo chake cha kwanzabarani Afrika jijini Nairobi

Kituo hicho kitajenga bidhaa na huduma zake kwa soko la Afrika na ulimwengu.

Haya yanajiri baada ya kampuni hiyo kubwa ya teknolojia kufichua mnamo Oktoba mwaka jana kupanga kuwekeza dola bilioni 1 katika miaka mitano ijayo.

Kituo hicho kitakuwa kitega uchumi cha pili kikubwa cha Google cha utafiti na maendeleo barani Afrika baada ya kuanzisha AI na kitovu cha utafiti nchini Ghana mnamo 2019.

Google ni kati ya makampuni makubwa ya kiteknolojia yanayoanzisha vituo vya uvumbuzi jijini Nairobi.

Wiki mbili zilizopita, muda mfupi baada ya Microsoft kuzindua kituo cha utafiti na maendeleo jijini Nairobi, Visa ilitangaza kuwa ilikuwa imeanzisha kituo chake cha kwanza barani Afrika.

Mwezi Oktoba mwaka jana, katika hafla ya Google kwa Afrika, Mkurugenzi Mtendaji Sundar Pichai alitangaza mpango wa kuwekeza dola bilioni 1 katika kipindi cha miaka mitano ijayo kusaidia ukuaji wa kidijitali barani Afrika.

Uwekezaji huu unalenga kuwezesha ufikiaji wa mtandao wa haraka na wa bei nafuu kwa Waafrika zaidi, kujenga bidhaa muhimu, kusaidia wajasiriamali na biashara ndogo ndogo na kusaidia mashirika yasiyo ya faida kuboresha maisha barani Afrika.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted