Ivory Coast: Tani 2 za Cocaine, yenye thamani ya zaidi ya Milioni 67, yakamatwa

Kukamatwa kwa kokeini imekuwa jambo la kawaida katika Pwani ya Atlantiki ya Afrika Magharibi,eneo linalotumika kwa usafirishaji wa dawa za kulevya kutoka Amerika Kusini kuelekea Uropa.

0

Polisi nchini Ivory Coast wamenasa zaidi ya tani 2 za kokeini yenye thamani ya takriban dola milioni 67.7, wizara ya mambo ya ndani ilisema Jumamosi.

Kokeini hiyo ilinaswa katika operesheni ya polisi iliyofanyika katika mji mkuu wa kibiashara wa Abidjan na mji wa bandari wa San Pedro, taarifa ya wizara ilisema.

Watu tisa wakiwemo raia wa Ivory Coast na raia wa kigeni wamekamatwa na uchunguzi unaendelea.

Mwaka mmoja uliopita tani moja ya kokeini ilikamatwa katika wilaya moja ya kaskazini mwa Abidjan.

Kukamatwa kwa kokeini imekuwa jambo la kawaida katika Pwani ya Atlantiki ya Afrika Magharibi,eneo linalotumika mara kwa mara kwa usafirishaji wa dawa za kulevya kutoka Amerika Kusini kuelekea Uropa.

Takriban tani 40 hupitia eneo hilo kila mwaka, kulingana na Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo. Kwa mujibu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu, mgawanyiko wa kisiasa wa nchi hiyo uliopo hivi sasa na kutokuwepo na udhibiti wa kutosha wa serikali katika eneo lake la kaskazini kunafanya biashara ya dawa za kulevya, pamoja na biashara haramu ya maliasili, kuenea zaidi

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted