Nigeria: Watu wenye silaha waua waumini katika shambulizi kanisani

Watu wenye silaha na vilipuzi walivamia kanisa la Kikatoliki na kufyatua risasi na kuua waumini kwenye kanisa kusini magharibi mwa Nigeria

0

Watu wenye silaha na vilipuzi walivamia kanisa la Kikatoliki na kufyatua risasi na kuua waumini kwenye kanisa kusini magharibi mwa Nigeria siku ya Jumapili na kuwajeruhi wengine, serikali na polisi walisema.

Ghasia katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Francis katika mji wa Owo katika Jimbo la Ondo zilizuka wakati wa ibada ya asubuhi katika shambulio la kusini-magharibi mwa Nigeria, ambapo wanajihadi na magenge ya wahalifu wanaendesha shughuli zao katika maeneo mengine.

Papa Francis alisema katika taarifa yake “kifo cha makumi ya waumini” watoto wengi, wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya Kikristo ya Pentekoste.

“Wakati maelezo ya tukio hilo yakifafanuliwa, Papa Francis aliombea waaathiriwa na kwa ajili ya nchi,” alisema.

Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo.

Sababu na idadi kamili ya vifo haikufahamika mara moja, lakini Rais Muhammadu Buhari alilaani “mauaji ya kinyama ya waumini.”

Msemaji wa polisi wa jimbo hilo Ibukun Odunlami alisema watu hao wenye silaha pia walishambulia kanisa hilo kwa vilipuzi na kusababisha vifo vya waumini idadi yao isiojulikana.

“Bado ni mapema kusema ni watu wangapi waliuawa. Lakini waumini wengi walipoteza maisha huku wengine wakijeruhiwa katika shambulio hilo,” aliiambia AFP.

Msemaji wa ofisi wa gavana wa Jimbo la Ondo alisema kuwa hawatatoa takwimu rasmi za majeruhi kwa sasa.

Lakini shuhuda aliyejitambulisha kwa jina la Abayomi, aliambia shirika la habari la AFP kuwa takriban waumini 20 waliuawa katika shambulio hilo.

“Nilikuwa nikipita eneo hilo nilisikia mlipuko mkubwa na milio ya risasi ndani ya kanisa,” alisema.

Alisema aliona angalau watu watano wenye silaha kwenye eneo la kanisa kabla ya kukimbilia usalama.

Mashambulizi kwenye sehemu za kidini ni nyeti sana nchini Nigeria ambapo mivutano wakati mwingine huzuka kati ya jamii katika nchi yenye Wakristo wengi wa kusini na kaskazini yenye Waislamu wengi.

Mashambulizi ya bunduki na mabomu ni nadra katika jimbo la Ondo, lakini jeshi la Nigeria linapambana na waasi wa jihadi kaskazini mashariki, magenge kaskazini magharibi na msukosuko wa kujitenga kusini mashariki.

Kundi la wanajihadi la Boko Haram kaskazini mashariki lililenga makanisa siku za nyuma kama sehemu ya mzozo wa Nigeria ambao umesababisha vifo vya watu 40,000 na wengine milioni 2 kuyahama makazi yao.

Mashambulio ya utekaji nyara ni ya kawaida katika maeneo mengi ya Nigeria lakini mashambulizi ya risasi kama vile vurugu za Jumapili ni nadra katika eneo la kusini-magharibi ambalo lina amani kiasi.

Gavana wa jimbo la Ondo Rotimi Akeredolu alisema shambulio la Jumapili lilikuwa ‘shambulio baya na la kishetani’ na kuviomba vyombo vya usalama kuwasaka washambuliaji.

Shambulio hilo linakuja siku moja kabla ya chama tawala cha APC kuanza mchujo wa mgombea wake katika uchaguzi wa 2023 kuchukua nafasi ya Buhari, kamanda wa zamani wa jeshi ambaye anastaafu baada ya mihula miwili ya uongozi.

Usalama utakuwa changamoto kubwa kwa yeyote atakayeshinda kinyang’anyiro cha kuitawala nchi hiyo yenye watu wengi zaidi barani Afrika na yenye uchumi mkubwa zaidi barani humo.

Maeneo ya kaskazini-magharibi na kaskazini-kati mwa Nigeria haswa yamezidi kukumbwa na magenge yenye silaha ambao huvamia vijiji na kulenga jamii na shule kwa mashambulizi makubwa ya utekaji nyara.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted