Rwanda inasema haijavunjika moyo baada ya ndege ya watafuta hifadhi ya Uingereza kufutiliwa mbali

Safari ya kwanza ya ndege ilipaswa kuondoka Uingereza kuelekea Rwanda Jumanne jioni lakini ilikatishwa baada ya uamuzi wa dakika za mwisho wa Mahakama ya Ulaya ya Haki za...

0

Serikali ya Rwanda ilisema Jumatano bado ina nia ya kuwapokea watu wanaotafuta hifadhi waliotumwa na Uingereza chini ya makubaliano yenye utata baada ya safari ya kwanza ya ndege kufutwa kufuatia uamuzi wa mahakama ya Ulaya.

“Hatujakatishwa tamaa na mabadiliko haya. Rwanda inasalia kujitolea kikamilifu kufanya ushirikiano huu ufaulu,” msemaji wa serikali Yolande Makolo aliiambia AFP.

“Hali ya sasa ya watu kufanya safari za hatari haiwezi kuendelea kwani inasababisha mateso mengi kwa wengi,” alisema

“Rwanda iko tayari kupokea wahamiaji hao watakapofika na kuwapa usalama na fursa katika nchi yetu.”

Safari ya kwanza ya ndege ilipaswa kuondoka kutoka Uingereza kuelekea nchi hiyo ya Afrika Mashariki Jumanne jioni lakini ilikatishwa baada ya uamuzi wa dakika za mwisho wa Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu.

Sera ya Uingereza ya kuwafukuza wanaotafuta hifadhi katika nchi iliyo umbali wa maelfu ya kilomita imetajwa kuwa “isiyo na maadili” na viongozi wa makanisa nchini Uingereza na kukosolewa vikali na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi na mashirika ya kutetea haki za binadamu.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted