Ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu DR Congo inasema waasi wa M23 wanapanga kuuteka mji muhimu

Wataalamu huru wanaoripoti kwa Umoja wa Mataifa kuhusu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo walisema Ijumaa kuwa waasi wa M23 wanapanga kuuteka mji wa mashariki wa Goma, DR Congo

0
Polisi wa Congo wakitafuta watu waliojipenyeza na silaha katika vizuizi vilivyowekwa huko Goma, Mei 28, 2022 huku mvutano kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Rwanda ukizidi, kuhusu madai yake ya kuunga mkono waasi wa M23 wanaondeleza mashambulizi Kivu Kaskazini. (Photo by Aubin Mukoni / AFP)

Wataalamu huru wanaoripoti kwa Umoja wa Mataifa kuhusu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo walisema Ijumaa kuwa waasi wa M23 wanapanga kuuteka mji wa mashariki wa Goma ili kupata mwafaka wa kisiasa.

Mapigano ya hivi majuzi kati ya waasi na wanajeshi wa Congo yamezidisha hali ya wasiwasi katika eneo hilo, huku serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ikiituhumu nchi jirani ya Rwanda kuwa inaunga mkono M23.

Rwanda imekanusha mara kwa mara shtaka hilo.

Pande zote mbili zimeshutumu kila mmoja kwa mashambulizli kwenye mipoaka yake.

katika ongezeko la hivi punde zaidi, wapiganaji wa M23 waliuteka mji wa Bunagana kwenye mpaka wa Uganda.

Ripoti ya timu ya kimataifa ya wataalam wa Umoja wa Mataifa kuhusu DRC, ya Juni 14 iliyochapishwa Ijumaa, ilipendekeza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya mpango wa kukaba njia ya kuingia Goma na hatimaye kuuteka mji huo.

Kulingana na mahojiano na wapiganaji sita wa M23, kiongozi wa kundi hilo Jenerali Sultani Makenga alipanga kuteka Bunagana na miji mingine miwili katika jimbo la Kivu Kaskazini mashariki “ili kukata barabara ya kimkakati ya Goma-Rutshuru, na kisha kuchukua Goma,” ripoti hiyo ilisema.

Nia ni kupata maafikiano ya kisiasa ambayo yanajumuisha msamaha, kurejesha mali, nyadhifa za kisiasa na kuunganishwa kwa wapiganaji wa M23 katika jeshi la Congo, kulingana na ripoti hiyo.

Goma ni kitovu muhimu cha kibiashara cha takriban watu milioni moja mashariki mwa DRC, ambayo iko kwenye mpaka wa Rwanda.

Wanamgambo wa Kitutsi wa Congo ambao ni miongoni mwa makundi mengi yenye silaha mashariki mwa DRC, M23 walijinyakulia umaarufu duniani mwaka 2012 walipouteka mji huo kwa muda mfupi.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted