Nyani apora mtoto mchanga wakati akinyonyeshwa na mama yake

Kundi la nyani waliopo katika hifadhi ya Gombe iliyopo kijiji cha Mwamgongo mkoani Kigoma, limevamia nyumba ya Shayima Faya (20) na kumpokonya mtoto mchanga wakati akimnyonyesha na kutokomea...

0

Kundi la nyani waliopo katika hifadhi ya Gombe iliyopo kijiji cha Mwamgongo mkoani Kigoma, limevamia nyumba ya Shayima Faya (20) na kumpokonya mtoto mchanga wakati akimnyonyesha na kutokomea naye porini ambapo baadaye mtoto huyo alifariki dunia.

Akizungumza leo Juni 20, 2021 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, James Manyama, amesema tukio hilo limetokea Juni 18, 2022 katika kijiji hicho.

Kamanda Manyanya amesema baada ya tukio hilo mwanamke huyo alipiga kelele kuomba msaada na majirani walijitokeza na kumdhibiti mnyama pori huyo ambaye alimtupa mtoto huyo chini akiwa tayari amejeruhiwa kichwani, usoni na kwenye mguu wa kushoto.

“Wananchi walifanikiwa kulikimbiza kundi hilo la nyani lililomvamia mwanamke huyo wakati akimnyonyesha wanaye na kufanikiwa kumpata mtoto akiwa amejeruhiwa lakini baada ya kufikishwa katika kituo cha afya Mwamgongo alifariki dunia,” amesema Manyama.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted