Afrika Kusini yarekodi kisa cha kwanza cha ugonjwa wa monkeypox

Shirika la Afya Duniani lilisema wiki iliyopita kwamba Ulaya imesalia kuwa kitovu cha mlipuko wa monkeypox duniani.

0
Picha hii iliyotolewa na Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa ilipigwa mwaka wa 1997 wakati wa uchunguzi wa mlipuko wa monkeypox, uliofanyika katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), AFP PHOTO / Brian W.J. Mahy, BSc, MA, PhD, ScD, DSc / Centers for Disease Control and Prevention ”

Afrika Kusini siku ya Alhamisi iliripoti kisa chake cha kwanza cha ugonjwa wa monkeypox na kujiunga na nchi zingine 40 ambazo zimegundua wagonjwa wanaougua ugonjwa huo.

“Mgonjwa ni mwanamume mwenye umri wa miaka 30 kutoka Johannesburg ambaye hana historia ya kusafiri, kumaanisha kwamba hii haiwezi kuhusishwa nay eye kuambukizwa ugonjwa huo kutoka nje ya Afrika Kusini,” Waziri wa Afya Joe Phaahla aliambia mkutano wa waandishi wa habari.

“Kwa kufanya kazi na mamlaka husika za afya, mchakato wa kutafuta watu waliokuwa karibu na mginjwa huyo umeanza.”

Dalili za awali za monkeypox kwa kawaida hujumuisha homa kali, nodi za limfu zilizovimba na upele unaofanana na tetekuwanga.

Ugonjwa huo kwa kawaida huwa si mkali na wagonjwa kwa kawaida hupona baada ya wiki mbili au tatu.

Shirika la Afya Duniani lilisema wiki iliyopita kwamba Ulaya imesalia kuwa kitovu cha mlipuko wa monkeypox duniani.

Shirika la afya la Umoja wa Mataifa linatazamiwa kufanya mkutano wa dharura siku ya Alhamisi ili kubaini kama kuainisha mlipuko wa monkeypox duniani kama dharura ya afya ya umma.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted