Nigeria yaidhinisha ubebeji wa bunduki ili kujilinda dhidi ya majambazi

Jimbo la Zamfara kaskazini mwa Nigeria litaruhusu watu kubeba bunduki ili kujilinda dhidi ya majambazi wenye silaha baada ya mamlaka kushindwa kuzuia ongezeko la utekaji nyara na mauaji.

0

Jimbo la Zamfara kaskazini mwa Nigeria litaruhusu watu kubeba bunduki ili kujilinda dhidi ya majambazi wenye silaha baada ya mamlaka kushindwa kuzuia ongezeko la utekaji nyara na mauaji.

Serikali imewaambia polisi kutoa leseni za bunduki “kwa wale wote wanaohitimu na wanaotaka kupata bunduki ili kujilinda,” Hudu Yahaya, msemaji wa gavana Bello Matawalle, alisema kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Inakusudiwa “kushughulikia mashambulizi ya hivi majuzi yanayoongezeka, utekaji nyara na kudai fidia kwa uhalifu unaotekelezwa kwa jamii zetu zisizo na hatia,” alisema.

Majimbo mengi katika eneo la kaskazini mwa Nigeria, likiwemo Zamfara, yamekuwa yakilengwa na wanamgambo wenye silaha na majambazi ambao wamekuwa wakitekeleza idadi kubwa ya utekaji nyara kwa ajili ya kuitisha fidia na mauaji.

Ghasia hizo zimewalazimu maelfu kuyakimbia makazi yao.

Uhalifu unaongezeka wakati huo huo mamlaka inapambana na waasi wa Kiislamu na wanakabiliwa na machafuko ya kujitenga katika maeneo mbalimbali ya nchi.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted