Somalia yatoa leseni za kwanza kwa benki za kigeni

Benki inayomilikiwa na serikali ya Banque Misr ya Misri na Ziraat Katilim ya Uturuki zitakuwa benki za kwanza za kimataifa kufanya kazi nchini humo,

0

Somalia ilisema Jumapili ilitoa leseni kwa benki mbili za kigeni huku taifa hilo la Pembe ya Afrika likifungua sekta hiyo kwa wakopeshaji wa kimataifa.

Benki inayomilikiwa na serikali ya Banque Misr ya Misri na Ziraat Katilim ya Uturuki zitakuwa benki za kwanza za kimataifa kufanya kazi nchini humo, Benki Kuu ya Somalia ilisema katika taarifa yake.

“Maombi  ya benki zote mbili kuhudmu Somalia yalichukua miezi ya mchakato wa kina,” ilisema, na kuongeza kuwa walipata ruhusa ya kuanzisha na kuendesha matawi.

“Zote ni benki imara ambazo zitaongeza thamani katika maendeleo ya sekta ya fedha ya Somalia na kuchangia ukuaji wa uchumi wetu,” taarifa hiyo ilimnukuu gavana wa Benki Kuu ya Somalia Abdirahman Mohamed Abdullahi.

Somalia ni moja ya nchi maskini zaidi duniani, huku zaidi ya asilimia 70 ya wakazi wake wakiishi chini ya dola 1.90 kwa siku, Somalia inajitahidi kujikwamua kutokana na miongo kadhaa ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Nchi hiyo yenye watu milioni 15 ina angalau nusu dazeni ya benki za biashara, huku baadhi zikitoa huduma kupitia mfumo wa hawala, mtandao usio rasmi wa uhamishaji fedha unaofanywa kupitia dhamana ya ana kwa ana.

Hawala ni mfumo wa bei nafuu na ni bora kutumia, hivyo kuruhusu pesa kuwekwa kwenye benki ya kigeni na kutumwa papo hapo kwa wapokeaji ambao wanapaswa kutoa maelezo ya msingi pekee ya utambulisho yanayolingana na yale yaliyotolewa na mtumaji.

Tangazo hilo la Jumapili linakuja wiki chache tu baada ya Rais Hassan Sheikh Mohamud kuchukua madaraka kufuatia uchaguzi ambao ulikuwa umechelewa kwa muda mrefu na mzozo wa kisiasa uliodumu kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Utawala mpya wa Somalia unakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja na njaa na uasi mkubwa wa kundi la wanajihadi la Al-Shabaab.

Mohamud ameapa kukabiliana na matatizo mengi ya Somalia ikiwa ni pamoja na kuboresha uchumi na kutoa huduma za kimsingi kwa watu.

Ukame mbaya katika eneo la Pembe ya Afrika umeacha takriban Wasomali milioni 7.1 — karibu nusu ya wakazi — wakipambana na njaa, huku zaidi ya 200,000 wakiwa kwenye ukingo wa njaa, kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa.

Al-Shabaab pia wanaendelea kuhatarisha maisha ya watu nchii humo wakifanya mashambulizi mwezi uliopita na kuwaua wanajeshi watatu katikati mwa Somalia, na kuweka dhahiri kazi ngumu inayowakabili viongozi wapya wa nchi hiyo.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted