Afrika Kusini: Polisi wawakamata watu wawili baada ya mashambulizi kwenye baa

Polisi wamewakamata watu wawili kuhusiana na moja kati ya matukio mawili ya ufyatuaji risasi kwenye baa ambayo yalisababisha vifo vya watu 19,

0

Polisi nchini Afrika Kusini walisema siku ya Jumatatu wamewakamata watu wawili kuhusiana na moja kati ya matukio mawili ya ufyatuaji risasi kwenye baa ambayo yalisababisha vifo vya watu 19, katika mauaji yaliyoshtua taifa hilo.

Kukamatwa kwa watu hao kumekuja huku kukiwa na uchunguzi wa ufyatuaji risasi wa Jumamosi usiku kwenye tavern katika mji wa mashariki wa Pietermaritzburg, katika jimbo la KwaZulu-Natal, ambapo watu wanne waliuawa na wanane kujeruhiwa wakati wanaume wawili walipowafyatulia risasi wateja kiholela.

Wizara ya polisi ilielezea kukamatwa kwa watu hao katika taarifa kama “hatua ya kwanza ya kuwaweka kizuizini wale wote ambao walipanga  umwagaji damu mkubwa nchini humo.”

Haikutoa maelezo yoyote zaidi.

Watu wengine 15 — miongoni mwao wanawake wawili — walipigwa risasi na kufa mapema Jumapili walipokuwa wakifurahia tafrija ya usiku katika kitongoji cha Soweto, karibu na Johannesburg, katika tukio tofauti.

Lirandzu Themba, msemaji wa wizara hiyo, aliliambia shirika la habari la AFP kuwa polisi wanaamini walioshikiliwa wanahusishwa  na ufyatuaji risasi wa Pietermaritzburg.

Ufyatulianaji wa risasi ni jambo la kawaida nchini Afrika Kusini, ambayo ina moja ya viwango vya juu zaidi vya mauaji duniani, yanayochochewa na vurugu za magenge na unywaji wa pombe.

Lakini mauaji ya kiholela katika wikendi yaliwaacha wachunguzi na mshangao.

“Kama taifa, hatuwezi kuruhusu wahalifu wa jeuri kututisha kwa njia hii, bila kujali ni wapi matukio kama haya yanaweza kutokea,” Rais Cyril Ramaphosa alisema katika taarifa yake Jumapili.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted