Sudan: Mwanamke, 20, kupigwa mawe hadi kufa kwa kosa la uzinzi

Mara ya mwisho kwa mwanamke kuhukumiwa kifo kwa kupigwa mawe kwa kosa la uzinzi nchini Sudan ilikuwa mwaka wa 2013

0

Mwanamke mmoja nchini Sudan atapigwa mawe hadi kufa kwa kupatikana na kosa la uzinzi katika kisa cha kwanza kama hicho kwa muda wa miaka 10.

Maryam Alsyed Tiyrab, 20, alikamatwa katika jimbo la White Nile nchini Sudan mwezi uliopita kabla ya kupatikana na hatia ya uzinzi na mahakama mnamo Juni 26.

Maryam – ambaye alikuwa amerejea nyumbani kwa familia yake baada ya kutengana na mumewe – anadai kuhojiwa na polisi na kulazimishwa kutoa ungamo kinyume cha sheria.

Jaji wa sharia aliamuru apigwe mawe hadi afe, uamuzi ambao amekata rufaa katika Mahakama Kuu ya Sudan.

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 20 anasema alinyimwa wakili na kwamba mahakama haikupata malalamiko ya polisi kabla ya kesi yake kuanza.

Nchini Sudan – ambayo inatumia sharia kama muundo wake wa kisheria – watu waliopatikana na hatia ya uhalifu wa Hudud, ambao ni pamoja na wizi, wizi katika barabara kuu, uzinzi na uasi, wanaweza kukatwa mikono na miguu, kuchapwa viboko au hata kuuawa na serikali.

Mara ya mwisho kwa mwanamke kuhukumiwa kifo kwa kupigwa mawe kwa kosa la uzinzi nchini Sudan ilikuwa mwaka wa 2013 – lakini mwanamke huyo alinusurika kifo wakati Mahakama Kuu ilipobatilisha uamuzi huo.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanataka Maryam aachiliwe mara moja.

Kituo cha Afrika cha Mafunzo ya Haki na Amani (ACJPS), chenye makao yake nchini Uganda kilitoa wito wa “kuachiliwa mara moja na bila masharti” kwa Tiyrab na kuishutumu Serikali ya Sudan kwa kukiuka sheria za ndani na kimataifa.

Katika taarifa yake, Kituo cha Afrika cha Mafunzo ya Haki na Amani (ACJPS) kilisema: “Kutumika kwa hukumu ya kifo kwa kupigwa mawe kwa kosa la uzinzi ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa, ikiwa ni pamoja na haki ya kuishi na kukataza mateso na ukatili, unyama au adhabu ya kudhalilisha.”

Kupiga mawe kama aina ya adhabu ya kifo bado inatekelezwa katika mataifa kadhaa ya sharia, ikiwa ni pamoja na Iran, UAE, Qatar, Mauritania, Saudi Arabia, Somalia na Yemen.

Mnamo Novemba mwaka jana, iliibuka kuwa Iran ilipanga kumhukumu kifo mume na mpenzi wake kwa uzinzi baada ya baba mkwe wa mwanaume kutaka wauawe, kulingana na ripoti.

Mke wa mwanamume huyo anasemekana kuwapa polisi klipu za video za uasherati wa mume wake mapema mwaka huu, lakini pia aliomba yeye na bibi yake waepushwe adhabu kali, vyombo vya habari vya nchini viliripoti.

Ni babake mke aliyetaka wawili hao wauawe na mahakama itoe uamuyzi huo kwa niaba yake, Shargh Daily iliripoti.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted