CDC: Amerika inaongoza kwa idadi ya visa vya monkeypox

Zaidi ya visa 3,800 vya monkeypox vimeripotiwa nchini Amerika, idadi kubwa zaidi katika nchi yoyote ulimwenguni, data ya afya ya serikali inaonyesha.

0

Zaidi ya visa 3,800 vya monkeypox vimeripotiwa nchini Amerika, idadi kubwa zaidi katika nchi yoyote ulimwenguni, data ya afya ya serikali inaonyesha.

Kuongezeka kwa idadi ya visa vya ugonjwa huo kumeripotiwa kusukuma utawala wa Biden kufikiria kutangaza dharura ya kiafya ya kitaifa.

Virusi hivyo tayari vimeainishwa kama dharura ya afya duniani na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Kufikia sasa, zaidi ya visa 18,000 zimeripotiwa katika nchi 75.

Kulingana na data iliyochapishwa mtandaoni na Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa vya Marekani (CDC), kufikia tarehe 25 Julai kulikuwa na visa 3,846 vilivyothibitishwa au kushukiwa vya monkeypox nchini Marekani.

Takwimu – ambayo inakuja huku kukiwa na ongezeko la upimaji wa ugonjwa huo pamoja na kuongezeka kwa milipuko ya virusi hivyo – Amerika sasa inaongoza kwa idadi ya viosa vya monkeypox ikishinda mataifa ya Uhispania, ambapo kesi 3,105 hadi sasa zimeripotiwa.

Nchi zingine mbili zilizo na idadi kubwa ya maambukizo, Ujerumani na Uingereza, zimeripoti visa 2,352 na 2,208, mtawaliwa.

Huku visa vya ugonjwa huo nchini Marekani vikiongezeka, gazeti la Washington Post mnamo tarehe 25 Julai liliripoti kwamba utawala wa Biden ulikuwa unazingatia kutangaza dharura ya afya ya umma.

Hatua hiyo itairuhusu serikali kutumia fedha za shirikisho kupambana na mlipuko huo, kuongeza uelewa wa umma na kukusanya data muhimu za afya.

Zaidi ya hayo, utawala unaripotiwa kujiandaa kutaja mratibu wa kusimamia shughuli za kukabiliana na ugojwa huo kutoka Ikulu.

Amerika ilithibitisha visa vya vya monkeypox kwa watoto mnamo Julai 22.

Mwitikio wa Amerika kwa virusi hadi sasa umekumbwa na uhaba wa chanjo na kusababisha wengine kulinganisha hali hiyo na mwanzo wa mlipuko wa janga la Covid-19 mapema 2020.

Huko Washington DC, kwa mfano, maafisa wameonya kwamba ‘ongezeko la haraka la visa’ pamoja na utoaji wa chanjo ‘wa chini wa chanjo,’ inamaanisha kwamba mamlaka lazima zipe kipaumbele wakazi walio katika hatari kubwa.

Jiji kwa sasa lina idadi kubwa zaidi ya watu walioambukizwa, na visa 172 vimeripotiwa katika wilaya hiyo.

Visa vingi vya monkeypox huwa hafifu, vikiwa na dalili za homa kali, nodi za limfu zilizovimba na malengelenge, upele au vidonda kama tetekuwanga.

Kufikia sasa, hakuna vifo kutokana na monkeypox vilivyoripotiwa nchini Amerika.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted