Ivory Coast yatangaza ugunduzi mpya wa mafuta na gesi

Kampuni ya Italia ya Eni imeripoti ugunduzi mpya wa mafuta na gesi asilia nchini Ivory Coast

0

Kampuni ya Italia ya Eni imeripoti ugunduzi mpya wa mafuta na gesi asilia nchini Ivory Coast na kuongeza uwezo wa akiba nyingine ya mafuta iliyopatikana mwaka jana kwa asilimia 25.

Mnamo Septemba 2021, nchi ilikuwa imetangaza kupatikana kwa mafuta yanayokadiriwa kuwa kati ya mapipa 1.5 na bilioni 2 ya mafuta na karibu futi za ujazo trilioni 1.8-2.4 za gesi.

Ugunduzi wa hivi punde katika pwani ya mashariki ‘unaongezeka kwa takriban asilimia 25’ ugunduzi uliotangazwa hapo awali, wizara ya madini, mafuta na nishati ilisema katika taarifa yake, na uchimbaji unatarajiwa kuanza mapema 2023.

Rais Alassane Ouattara amesema anataka Ivory Coast iwe mzalishaji mkuu wa mafuta.

Pato la sasa la taifa hilo la Afrika Magharibi ni la wastani, karibu mapipa 30,000 kwa siku.

Makampuni ya kimataifa yakiwemo kampuni kubwa ya Ufaransa Total na Tullow Oil ya Uingereza pia yametangaza uvumbuzi muhimu wa hifadhi ya mafuta ya Ivory Coast katika miaka ya hivi karibuni.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted