Kenya: Idara ya upelelezi yaanza kuchunguza madai ya mbunge kuhusu wizi wa kura.

Mbunge huyo mapema Jumatatu alidai kuwa, serikali inapanga kusafirisha shehena 40 ya karatasi zilizotiwa alama ya kupiga kura

0

Idara ya upelelezi nchini Kenya imeanza uchunguzi kuhusu madai ya mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria kuwa serikali inapanga njama ya kuiba kura kwa niaba ya mgombea wa azimio Raila Odinga.

Mbunge huyo mapema Jumatatu alidai kuwa, serikali inapanga kusafirisha shehena 40 ya karatasi zilizotiwa alama ya kupiga kura katika meneo tofauti kutoka ikulu ya Nakuru kabla ya uchaguzi wa jumanne.

“Watu wa Uasin Gishu. Mojawapo ya lori itakayotoka kutoka ikulu ya Nakuru kuelekea Eldoret ni KcW853T”  Alisema mbunge huyo kupitia mtandao wake wa Facebook.

Idara ya DCI sasa inamtaka mbunge huyo kufika katika kituo cha polisi kilicho karibu kuandikisha taarifa kuhusu madai yake.

”Tumepata taarifa kuhusu ujumbe ulioandikwa katika mitandao ya kijamii na mbunge wa Gatundu Moses Kuria akiibua madai kwamba serikali inapanga jinsi ya kuiba kura kwa niaba ya mgombea wa Azimio Raila Odinga.” Alisema mkurugenzi wa DCI katika taarifa.

Idara ya upelelezi inamtaka mbunge huyo kufika katika kituo cha polisi au ofisi za idara ya upelelezi uliokaribu naye haraka iwezekanavyo, ili asaidie katika uchunguzi wa kina na wa hara katika madai hayo.

Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria.
In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted