Mlipuko wa Ebola wazuka tena nchini DRC       

Kwa mujibu wa WHO uchunguzi umeonyesha kuwa kisa hicho kinahusiana na milipuko miwili iliyodumu kwa muda mrefu nchini humo ya majimbo ya Kivu Kaskazini na Ituri.

0

Maafisa wa afya nchini Jamhuri ya Kimokrasia ya Congo DRC wametangaza kuzuka tena kwa ugonjwa wa Ebola baada ya kisa kimoja kuthibitishwa kwenye jimbo la Kivu Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na shirika la afya la Umoja wa Mataifa mjini Brazzaville na Kishasa mwanamke mwenye umri wa miaka 46 alifariki dunia tsrehe 15 Agosti mjini Beni jimboni humo na alipatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya Beni alikolazwa ambapo baadaye alionyesha dalili za Ebola.

Shirika hilo linasema vituo vyote viwili vya kitaifa vya uchunguzi wa kitabibu Beni na Goma INRB vinethibitisha kuwa ni virusi vya Ebola baada ya kufanyia uchunguzi sampuli iliyochukuliwa kwa mgonjwa.

Kwa mujibu wa WHO uchunguzi umeonyesha kuwa kisa hicho kinahusiana na milipuko miwili iliyodumu kwa muda mrefu nchini humo ya majimbo ya Kivu Kaskazini na Ituri.

Akizungumzia mlipuko huo mkurugenzi wa WHO kanda ya Africa Dkt.Matshidiso Moeti amesema “Kujirudia kwa milipuko ya Ebola kunatokea mara nyingi DRC hali ambayo inatia hofu. Hata hivyo mamlaka za afya Kivu Kaskazini zimefanikiwa kuikomesha milipuko kadhaa na kuendeleza utaalam huo bila shaka kutasaidia kuudhibiti mlipuko huu wa sasa haraka.”

Wafanyakazi wa WHO na mamlaka za afya DRC wanashirikiana kutafuta chazo cha kusambaa kwa ugonjwa huo na tayari wamebaini watu 160 ambao walikutana na marehemu na wako chini ya uangalizi.

Pia uchunguzi unaendelea kubaini hali ya chanjo ya kisa kilichothibitishwa.

Shirika la afya duniani linasema kuna akiba ya dozi 1000 za chanjo ya Ebola ya rVSV-ZEBOV nchini humo na dozi 200 kati ya hizo zitapelekwa Beni wiki hii.

Mzunguko wa chanjo kwa watu waliokutana na mgonjwa na waliokutana na watu hao utaanza hivi karibuni ili kudhibiti kusambaa kwa virusi hivyo na kulinda maisha ya watu.

Mlipuko wa mwisho mjini Beni jimboni Kivu Kaskazini ulidhibitiwa ndani ya muda wa miezi miwili na ulikomeshwa tarehe 16 Desemba 2021.

Kwa wakati huo kulikuwa na visa 11 ambapo 8 kati ya hivyo vilithibitishwa, vitatu vilidhaniwa na ulijumuisha vifo 6.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted