JTI kununua kilo milioni 30 za tumbaku Tanzania
Ahadi hiyo imetolewa jana Jumatatu, Septemba 26, 2022 na Rais na Mtendaji Mkuu wa JTI, Masamichi Terabatake mbele ya Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa, aliyetembelea ofisi zao, ili kuwahakikishia utekelezaji wa mazungumzo yaliyofanyika wakati wa mkutano wa TICAD 8, jijini Tunis, Agosti, mwaka huu.