Rais mstaafu Uhuru Kenyatta kutohudhuria mkutano wa kurejesha amani Ethiopia

Mkutano huo unafaa kufanyika nchini Afrika Kusini kuanzia kesho chini ya uongozi wa aliyekuwa rais wa Nigeria Olesgun Obasanjo.

0
Rais mstaafu wa Kenya Uhuru Kenyatta

Rais mstaafu wa Kenya Uhuru Kenyatta hatohudhuria mazungumzo ya amani iliyoitishwa na Umoja wa Afrika(AU)  kuhusu mzozo wa Ethiopia.

Mkutano huo unatarajiwa kuanza siku ya jumamosi nchini Afrika Kusini. Katika waraka aliyomwandikia mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Mousa Faki Mahamat, Kenyatta amesema mkutano huo umejiri wakati akiwa na shughuli alizokuwa amepangia awali.

Rais huyo mstaafu wikendi hii alitarajiwa kujiunga na vikosi vya umoja wa Afrika katika mazungumzo ya amani itakayoongozwa na aliyekuwa rais wa Naigeria Olesgun Obasanjo pamoja na aliyekuwa makamo wa rais wa Afrika Kusini  Phumzile Mulambo Ngcuka nchini Afrika Kusini.

Hii ingekuwa mkutano wa kwanza kwa rais mstaafu kuhudhuria tangu kuchaguliwa kwake na mrithi wake William Ruto kuwakilisha taifa la Kenya katika mazungumzo hayo ambayo yanalenga kuzima mzozo wa miaka miwili kati ya vikosi vya Tigray na serikali ya Ethiopia.

Hata hivyo, sasa ni bayana kuwa kiongozi huyo hatohudhuria mkutano huo ambao unajiri mwezi mmoja baada ya mapigano mapya kuzuka kati ya pande hizo mbili kufuatia miezi kadhaa ya hali ya utulizo.

Katika waraka kwa mwenyekiti wa umoja wa Afrika Mousa Faki Mahamat leo hii, Kenyatta ameelezea kuwa hatawezeshwa kuhudhuria mkutano huo kwani umegongana na shughuli ambazo alikuwa amepanga hapo awali.

Kiongozi huyo wa Kenya ameomba kupewa kanuni na masharti za kushiriki mazungumzo sawia ndiposa aweze kujiandaa vilivyo kwa ajili ya kuhudhuria katika siku za usoni.

Vilevile Kenyatta ameelezea imani yake kuwa mzozo huo utafikia kikomo na kuirai serikali ya Uhabeshi na uongozi wa vikosi vya Tigray kushiriki katika juhudi zilizoanzishwa na umoja wa Afrika.

Kufuatia vita hivyo vilivyoanza novemba mwaka jana, huduma muhimu kama vile afya, mtandao na umeme zimetatizika huku watu takriban milioni tano wakiathirika kutokana na vita hivyo.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted