Mwanawe Odinga, Winnie Odinga kuwakilisha Kenya katika bunge la Afrika Mashariki

Winnie Odinga, Binti mdogo wa Raila Odinga akiibuka wa pili kwa kura 247, jambo ambalo linamfungulia njia ya kuwakilisha taifa la Kenya kwa muhula wa miaka mitano katika...

0
Mwana mdogo wa kiongozi wa upinzani Kenya, Winnie Odinga. Picha-@Winnie_Odinga

Viongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga na Kalonzo Musyoka wameibuka kuwa washindi wakubwa zaidi katika uchaguzi wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) baada ya wanao kuingia kwenye orodhaa ya mwisho.

Licha ya juhudi za kuzima ndoto za wawili hao kufika katika bunge la EALA iliyoko Arusha kwa misingi kuwa “wazee” wao wamekuwa kwenye siasa za uongozi wa kitaifa miaka nenda rudi, waliibuka kidedea katika kinyang’anyiro hicho kikali.

Katika uchaguzi huo ambao uliendeshwa katika bunge la kitaifa na seneti, mwanawe Kalonzo Musyoka- Kennedy Musyoka alipata kura 262 ambazo zilikuwa hesabu ya juu zaidi kati ya walioteuliwa na muungano wa Azimio la Umoja One Kenya.

Kwa upande mwingine Winnie Odinga, Binti mdogo wa Odinga akiibuka wa pili kwa kura 247, jambo ambalo linamfungulia njia ya kuwakilisha taifa la Kenya kwa muhula wa miaka mitano katika bunge hilo lililoko Arusha mjini.

Katika taarifa pindi tu baada ya kuchaguliwa Winnie, alitwaa ushindi wake kuelekea katika bunge la Afrika Mashariki kwa wafuasi 49 waliopoteza maisha mwaka wa 2017.

Winnie aliwashukuru wafuasi waliosimama na familia yake kwa miaka mingi na kusema kuwa ni bahati mbaya kuwa watu hao 49 walipoteza maisha wakimkaribisha babake (Raila Odinga) nchini.

Winnie Odinga akipokea cheti cha kuchaguliwa kama mjumbe wa bunge la EALA

Winnie ameahidi kuendelea kutetea haki za watu katika Bunge la eneo la Afrika Mashariki lenye makao yake makuu nchini Tanzania.

“Miaka mitano iliyopita sawa na leo, tulipotoka uwanja wa ndege wa JKIA, watu 49 walipoteza maisha. Mimi bado niko hapa kwa neema ya Mungu. Leo hii, nimechaguliwa kuwa mwanachama wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA)

“Nimenyenyekezwa. Ninashukuru. Niko tayari. Hii ni kwa wote tuliowapoteza njiani. Hakuna mimi bila wewe,” alisema Winnie.

Baadhi ya viongozi wa muungano wa Kenya Kwanza hata hivyo, walikuwa wameahaidi kushawishi wabunge wa muungano huo kupiga kura dhidi yake.

Winnie akizungumza katika mahojiano na kituo kimoja cha runinga nchini Kenya hivi majuzi, alisema jina lake la familia limemfanya “kunyanyaswa” na “kuteswa” na halikuwa faida ya kisiasa kama wanavyodai baadhi ya wakosoaji wake.

Kiongozi wa Azimio Raila Odinga na mwawe Winnie Odinga.

Bi Odinga alidai kuwa wakosoaji wake hawataki kuangazia anachoweza kufanya kwa sababu ya kuwa babake ni nani.

Hata hivyo, alisadiki kwamba jina hilo pia limekuwa Baraka kwake, kwani limemruhusu kusafiri ulimwenguni na kuelewa jinsi bara la Afrika linaweza kufanya kazi pamoja.

Winnie alichaguliwa kutoka muungano wa Azimio la Umoja pamoja na aliyekuwa mbunge Kanini Kega, mfanyibiashara wa Mombasa Suleiman Shahbal na mwanawe Kalonzo Musyoka, Kennedy Kalonzo.

EALA ni bunge la kutunga sheria cha jumuiya ya kikanda baina ya serikali,Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), na wanachama wanawakilisha mataifa yao kwa muhula wa miaka mitano.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted