Atwoli Amechaguliwa Makamu wa Rais wa ITUC kwa Awamu ya Nne

Uteuzi wa Atwoli uliidhinishwa kwa kauli moja na zaidi ya wajumbe 2000 na kufungua njia kwa muhula wake wa miaka mine katika ITUC, ambayo ina makao yake makuu...

0
Katibu mkuu wa COTU Francis Atwoli

Katibu Mkuu wa Muungano wa vyama vya wafanyikazi (COTU) Francis Atwoli amechaguliwa tena kwa muhula wa nne katika nafasi ya makamu wa rais wa shirikisho la vyama vya wafanyikazi Duniani (ITUC).

Atwoli alichaguliwa katika wadhifa huo katika Kongamano la 5 la shirika la vyama vya wafanyikazi linaloendelea huko Melbourne, Australia, huku bodi hiyo ikijivunia uanachama wa zaidi ya watu milioni 200 waliotolewa kutoka nchi 163.

Uteuzi wa Atwoli uliidhinishwa kwa kauli moja na zaidi ya wajumbe 2000 na kufungua njia kwa muhula wake wa miaka mine katika ITUC, ambayo ina makao yake makuu mjini Brussels, Ubelgiji.

“Nafasi ambayo mmenipa asubuhi ya leo sio rahisi. M       nanituma kupigania wanaume na wanawake wanaofanya kazi duniani kote. Sitawaangusha kamwe. Nitasimamia maslahi yenu na kuweka maisha yangu kwa ajili yenu kila mara.” Atwoli alisema.

Aidha alimhakikishia katibu mkuu mpya uungwaji mkono kutoka COTU (Kenya) katika kuhakikisha anatekeleza malengo yake.

Atwoli hapo awali alichaguliwa, liba kupingwa kwa kamati ya sifa ya wanachama saba, ndani ya usanifu wa ITUC ambayo huamua ni nani anahitimu kuwa mjumbe wa shirikisho.

Kamati pia inaripoti kuhusu muundo wa wajumbe mbalimbali kwa kila nchi pamoja na kiwango cha uwezo wao wa kupiga kura.

Kando na hayo, Atwoli alichaguliwa kuwa mjumbe wa Baraza kuu la ITUC kuwakilisha kanda la Afrika Mashariki, baada ya kupendekezwa na mjumbe kutoka Tanzania na kuungwa mkono na viongozi wa vyama vya wafanyikazi kutoka Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia naa Mauritious miongoni mwa wengine.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted