Jinsi safari ya Biden kwenda Ukraine ilivyofanywa kisiri

Maafisa walikuwa wamekanusha kuwa Biden angezuru Ukraine wakati wa safari yake ya kuelekea Ulaya mashariki.

0

Safari ya siri ya Biden kwenda Ukraine ilifanywa kupitia treni kutoka mpaka wa Poland, gazeti la New York Times linaripoti.

Ziara ya Kyiv ilifanywa kisiri kwa sababu ya tahadhari ya kiusalama.

Ripoti pia zinasema kwamba Biden aliondoka Washington bila taarifa baada ya yeye na mkewe Jill kula chakula cha jioni kwenye mkahawa Jumamosi usiku.

Maafisa walikuwa wamekanusha kuwa Biden angezuru Ukraine wakati wa safari yake ya kuelekea Ulaya mashariki.

Gazeti la The New York Times linasema: “Hakika, Ikulu ya Marekani Jumapili usiku ilitoa ratiba ya hadharani Jumatatu ikimuonyesha rais bado yuko Washington na kuondoka jioni kuelekea Warsaw, wakati alikuwa tayari ameanza safari.”

Kabla ya mkutano na waandishi wa habari, Joe Biden alifanya mazungumzo na Volodymyr Zelensky na kusema kwamba “anatazamia kujadili ulimwengu” pamoja naye.

Pia aliwasifu raia wa Ukraine kwa mapigano yao ya “kishujaa” – licha ya ukosefu wa uzoefu wa kijeshi. Alisema: “Tena cha kustaajabisha ni kwamba watu wa Ukraine ni raia wa kawaida, wachapakazi, ambao hawakuwahi kupata mafunzo ya kijeshi, lakini jinsi walivyopiga hatua ya kishujaa ni jambo ambalo na ulimwengu wote unajivunia.”

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted