Mgombea wa useneta wa Nigeria auawa kwa kupigwa risasi na mwili wake kuchomwa moto

Wasaidizi wake waliokuwa pamoja naye pia waliuawa kwa kupigwa risasi kabla ya gari lao kuchomwa moto huku miili ikiwa ndani, vyombo vya habari vya eneo hilo vinaripoti.

0

Mgombea wa kiti cha useneta nchini Nigeria ameuawa kwa kupigwa risasi siku ya Jumatano na mwili wake kuchomwa moto na washambuliaji alipokuwa akitoka kwenye mkutano wa kampeni katika jimbo la kusini la Enugu.

Shambulio dhidi ya Oyibo Chukwu wa Chama cha Labour lilitokea siku tatu kabla ya uchaguzi mkuu wa Jumamosi ambao unaelezwa kuwa uchaguzi wenye ushindani mkubwa zaidi nchini humo katika kipindi cha miaka 24.

Wasaidizi wake waliokuwa pamoja naye pia waliuawa kwa kupigwa risasi kabla ya gari lao kuchomwa moto huku miili ikiwa ndani, vyombo vya habari vya eneo hilo vinaripoti.

“Wanachama wa chama chetu wanalengwa kuuawa na vyama vya siasa ambavyo vilihisi kutishiwa na kuongezeka kwa Chama cha Labour katika jimbo hilo na wanahofia kuwa wanaweza kushindwa katika uchaguzi wa Jumamosi,” alisema Chijioke Edeoga, mgombea wa kiti cha ugavana katika jimbo hilo.

Chama cha Labour hakijatoa maoni yoyote kuhusu shambulio hilo, lakini mgombea wake wa urais Peter Obi amekuwa akiwataka wafuasi wake kupiga kura “kwa usahihi, kwa amani na matumaini”

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted