Kevin De Bruyne Ameteuliwa Nahodha Wa Timu Ya Taifa Ya Ubelgiji

Kiungo wa kati wa Manchester city Kevin De Bruyne amethibitishwa kuwa nahodha mpya wa timu ya taifa ya Ubelgiji kufuatia kustaafu kwa Eden Hazard.

0

Kiungo wa kati wa Manchester city Kevin De Bruyne amethibitishwa kuwa nahodha mpya wa timu ya taifa ya Ubelgiji kufuatia kustaafu kwa Eden Hazard.

Hazard aliamua kustaafu soka ya kimataifa baada ya Ubelgiji kuondolewa katika Kombe la Dunia la 2022 nchini Qatar mapema kinyume na matarajio yake, jambo ambalo pia lilimfanya Kocha mkuu Roberto Martinez kuondoka.

 Mrithi wake Martinez, Domenico Tedesco alibidi kujaza pengo la Hazard. Meneja huyo mwenye umri wa miaka 37 bila kupoteza muda alimdhibitisha De Bruyne kuwa nahodha mpya wa Ubelgiji kabla ya kampeni yao ya kufuzu Euro 2024, huku nyota huyo wa Manchester City akijivunia kuichezea taifa lake mara 97 na mabao 25 ​​katika ngazi ya kimataifa.

De Bruyne alisema amefurahishwa na uteuzi huo na yuko sawa na jukumu la kuongoza timu hiyo yenye Talanta hususan ya wachezaji wachanga sana duniani.

 “Ni heshima kwangu kutajwa na kuiwakilisha nchi kwa njia hii,” alisema De Bruyne

“Nina karibu miaka 32. Sijawahi kufikiria kustaafu kimataifa. Nafikiri bado ninaweza kuleta kitu mezani na kuwasaidia vijana.” Alisema Hazard

Kipa wa Real Madrid Thibaut Courtois na mshambuliaji wa Inter Romelu Lukaku waliteuliwa kuwa makamu wa manahodha. Hii si mara ya kwanza kwa De Bruyne kuvaa kitambaa hicho, alifanya hivyo mara kadhaa hapo awali, ikiwa ni pamoja na dhidi ya Croatia katika mchezo wao wa mwisho wa hatua ya makundi wa Kombe la Dunia la 2022.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted