Rwanda yaonya kuhusu ‘mauaji ya kimbari’ mashariki mwa DRC

Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda Vincent Biruta amesema kwamba nchi yake inahofu kuhusu uwezekano wauliopo wa “mauaji ya kimbari’’ dhidi ya raia wanazungumza Kinyarwanda mashariki mwa...

0

Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda Vincent Biruta amesema kwamba nchi yake inahofu kuhusu uwezekano wauliopo wa “mauaji ya kimbari’’ dhidi ya raia wanazungumza Kinyarwanda mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Akihutubia Kikao cha kitaifa cha jukwa la mashauriano cha kisiasa, Alhamisi, Bw Biruta aliilaumu jamii ya kimataifa kwa kushindwa kuchukua hatua kuzuia kuongezeka kwa ghasia , licha ya ripoti kadhaa kutolewa pamoja na “ushahidi unaoonyesha ukweli wa uwezekano wa mauaji ya kimbari”.

“Kutambua mauaji ya kimbari kunakwenda sambamba na uwajibikaji wa kuyazuia yasitokee. Sababu baadhi ya wadai wa kimataifa wanasita kuhusu kutambua mauaji ya kimbari ambayo yanapangwa katika DRC ni kwasababu kuyatambua unakwenda sambamba na uwajibikajiwa kuingilia kati na kuyazuia ,” alisema Bw Biruta.

“Wanakwepa huo uwajibu lakini tunaendelea kuwakumbusha ,” aliongeza.

Hii inakuja wakati DRC ikiendelea kuishutumu Rwanda kuwaunga mkono waasi wa M23 – katika mzozo wa kivita wa muongo mmoja mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo . Rwanda imekuwa ikikanusha dai hilo mara kwa mara.

Serikal ya Kigali pia imekuwa ikiishutumu Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo kwa kuwaunga mkono waasi wa kundi la Democratic Forces for the Liberation of Rwanda (FDLR), ambalo linajumuisha washukiwa wa mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994.

Mwezi Disemba mwaka jana wavuti wa gazeti la serikali ya Rwanda ulisema kauli za chuki na mauaji yanayowalenga Watutsi na raia Wacongo wanaozungumza Kinyarwanda katika DRC yanaweza kuwa kiashiria cha uwezekano wa mauaji ya kimbari.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted