Jinsi ya kuzuia ugonjwa wa Malaria

Malaria ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea vinavyoambukizwa kwa binadamu kwa kuumwa na mbu

0
Wanafunzi wakiwa na mabango wakati wa hafla ya kuadhimisha Siku ya Malaria Duniani katika hospitali ya serikali viungani mwa Amritsar mnamo Aprili 25, 2022. (Picha na Narinder NANU / AFP)

Tarehe 25 Aprili inaadhimishwa kama Siku ya Malaria Duniani. Malaria ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea vinavyoambukizwa kwa binadamu kwa kuumwa na mbu. Watu walio na malaria huwa na homa kali, hupata baridi kali na huhisi kuumwa sana. Hebu tuangalie sababu, dalili za malaria na jinsi ya kuzuia ugonjwa huo. Mbali na homa na baridi, malaria pia husababisha maumivu ya kichwa, kichefuchefu, kutapika, maumivu ya misuli, uchovu, maumivu ya kifua, kikohozi na jasho jingi.

Jinsi malaria inavyosababishwa na jinsi ya kutambua dalili ya kwanza
Unapata malaria mbu aliyeambukizwa vimelea anapokuuma na kuhamisha vimelea hivyo kwako. Huwezi kupata malaria kwa kuwa karibu na mtu aliye na ugonjwa huo.

Malaria pia inaweza kuenea kutoka kwa mama hadi kwa mtoto ambaye hajazaliwa, kwa kutiwa damu mishipani na kwa kuchangia sindano zinazotumika kudunga dawa.

Kuzuia Malaria

Malaria inaweza kuzuiwa kwa kuepuka kusafiri kwenda sehemu ambazo matukio ya ugonjwa huo ni makubwa – kama vile maeneo ya tropiki. Walio katika hatari kubwa ya kuugua malaria ni pamoja na watu wazima wazee, watoto wadogo na watoto wachanga, wajawazito na watoto wao ambao bado hawajazaliwa, wasafiri wanaotoka maeneo ambayo hakuna malaria.

Ili kujikinga na malaria, hakikisha unavaa nguo zinazokufunika ipasavyo, hasa ikiwa unaenda kwenye maeneo yenye unyevunyevu ambapo mbu wanaweza kuzaliana. Weka dawa za kuzuia wadudu kwenye ngozi yako na hata kwenye nguo. Katika nyakati ambapo matukio ya malaria ni mengi katika mazingira yako, lala chini ya chandarua.

Yeyote anayeonyesha dalili za malaria anapaswa kwenda kuchunguzwa mara moja. Uchunguzi wa vimelea ni muhimu kwa utambuzi wa malaria.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted