Donald Trump athibitisha kuwa hatashiriki mijadala ya urais ya chama cha Republican

"Umma unanijua mimi ni nani na nilikuwa na Urais gani wenye mafanikio," Bw Trump, 77, aliandika kwenye kwenye mtandao wa kijamii.

0

Donald Trump amethibitisha kuwa hatashiriki mijadala ya urais ya chama cha Republican na wapinzani wake katika kinyang’anyiro cha kuwania Ikulu ya White House.

Rais huyo wa zamani alisema kura ya maoni ya hivi punde ilionyesha kuwa alikuwa na idadi “ya kutosha kuwa maarufu” mbele ya watu wengine wanaotarajiwa kuteuliwa kugombea urais wa chama hicho katika uchaguzi wa 2024.

“Umma unanijua mimi ni nani na nilikuwa na Urais gani wenye mafanikio,” Bw Trump, 77, aliandika kwenye kwenye mtandao wa kijamii.

Mjadala wa kwanza wa mchujo wa urais wa chama cha Republican utakuwa tarehe 23 Agosti.

Mjadala wa pili unaweza kufanyika siku inayofuata. Angalau mijadala miwili zaidi inatarajiwa katika miezi ijayo.

Upigaji kura katika uchaguzi wa mchujo wa chama cha Republican utaanza katika jimbo la Iowa tarehe 15 Januari 2024, lakini kuna uwezekano wa mijadala zaidi kufanyika.

Kura za maoni za hivi karibuni zimeonyesha mara kwa mara kuwa Bw Trump – ambaye anakabiliwa na mashtaka kadhaa ya jinai – kwa sasa ndiye anayeongoza miongoni mwa wagombea wengine wanaotarajiwa kuteuliwa na chama cha Republican, kugombea urais.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted