, ,

“Hamkuwa Na Kosa La Kunihukumu” – Lissu Aishambulia Mahakama Kwa Kutengeneza Kosa Jipya Kwa Maelekezo Ya Kisiasa

Wadh Kassim Avatar

LISSU
“Leo ni Siku ya 577 nikiwa gerezani kwa kosa la Uhaini ndio kosa pekee lilitamkwa katika Katiba na ndio kosa kubwa kwa nchi hii. Kwa siku 577 nimeitwa mhaini, kosa ambalo kwa mujibu wa kifungu cha 39(2d) adhabu yake inaweza kuwa kifo. Baada ya siku 577 za hilo wingu jeusi la adhabu ya kifo kudidimia kwenye kichwa changu leo Waheshimiwa majaji mmeniita mchochezi kosa ambalo halina adhabu na wakili.

Mkuu wa serikali anahangaika kutafuta adhabu yake.

Maana yake ni nini, kosa nililoshtakiwa nalo halikua kosa na nyinyi Waheshimiwa majaji mmesema halikua kosa. Kwa hiyo nilikaa siku 577 bila ya kuwa na kosa lolote na Waheshimiwa majaji kauli yenu halikua kosa imekubaliana na ushahidi wangu na msimamo wangu kwamba hakukua na kosa lolote.

Kuna kitu kimoja mlikua hamjakisema, hii ilikua ni kesi ya kisiasa tu kugeuza mahakama ya jinai kuwa uwanja wa kisiasa. Kwa sababu ni kesi ya kisiasa inabidi visababu vitengenezwe vya kumfunga huyu mgomvi wetu wa kisiasa na visababu vyenyewe ni kosa la Uchochezi ambalo nyinyi Waheshimiwa majaji mmelitengeneza, sikushtakiwa nalo, nilishtakiwa nje ya Uhaini nilishtakiwa kwa kusambaza taarifa za uongo. Na Waheshimiwa majaji mmefanya hilo kwa sababu ya maelekezo ya kisiasa.

Hana kosa lakini isionekane ameachiwa hivihivi kwa hiyo tafuteni vijisabu ndicho mlichokubaliana na ninajua kuna hukumu, mmeshakubaliana ninajua.

Kwa bahati mbaya sana Waheshimiwa majaji mmefanya kile ambacho Mahakama ya Kenya ilikifanya 1954 mzee Jomo Kenyatta na wenzake.”

Our Correspondent Avatar