Bajeti ya Tanzania kupigiwa kura leo
Wabunge wanapata fursa ya kupiga kura baada ya siku saba za majadiliano tangu bajeti hiyo ilipowasilishwa bungeni jijini Dodoma Juni 13 mwaka huu, ikiwa ni bajeti ya nne.
Wabunge wanapata fursa ya kupiga kura baada ya siku saba za majadiliano tangu bajeti hiyo ilipowasilishwa bungeni jijini Dodoma Juni 13 mwaka huu, ikiwa ni bajeti ya nne.
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amewataka Watanzania kuacha matumizi holela holela ya Dawa ili kuepuka usugu wa vimelea dhidi ya dawa hususani za antibaotik kushindwa kufanya kazi ipasavyo na kugharimu maisha na nguvu kazi ya Taifa.
Jana Juni 18, 2024 Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson, alilitangazia bunge na kutoa amri chini ya mamlaka aliyonayo ya kumfikisha mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina kutokana na kwamba amelidharau bunge na mamlaka ya Spika.
Serikali imezindua ujenzi wa majengo pacha ya ghorofa 22 kila moja jijini Nairobi, Kenya, yatakayotumika kama Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini humo na kitega uchumi kwa ajili ya kuongeza fedha za kigeni.
Kesi hiyo imeanza kusikilizwa upya baada ya Mahakama ya Rufani iliyoketi Mwanza mbele ya majaji watatu, Ferdinand Wambali, Issa Maige na Leila Mgonya kutengua hukumu ya kesi hiyo na kuamuru ianze kusikilizwa upya, baada ya kubaini kasoro za kisheria katika mwenendo wa kesi hiyo Mahakama Kuu.
Akiongea Jijini Dar es salaam leo June 12,2024, Waziri Kivuli wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wa ACT Wazalendo, Rahma Mwita amesema Serikali ya CCM imekuwa na utamaduni wa kutovumilia maoni, mitazamo na fikra tofauti zinazotolewa na Wananchi kuhusu Viongozi na sera zao, na mara zote inatumia hila za namna tofautitofauti ili kutimiza dhamira hiyo kandamizi.
Kwa mwezi huu wa Juni bei ya rejareja ya mafuta ya petroli kupitia Bandari ya Dar es Salaam imeshuka kwa shilingi 53 na kufikia shilingi 3,261 kwa lita moja, ikilinganishwa na bei ya mwezi Mei iliyokuwa shilingi 3,314.
Ubalozi wa Tanzania nchini Korea Kusini umesema Tanzania haijasaini mkataba wowote na Jamhuri ya Korea unaohusu Bahari wala Madini katika ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan inayoendelea nchini humo.
Iwapo chama cha African National Congress (ANC) kitathibitishwa kuwa kimeshuka chini ya asilimia 50 ya kura, kitalazimisha chama kutafuta washirika wa muungano ili kuchaguliwa tena kuunda serikali mpya.
Mfumo Tovuti ya tume ya uchaguzi ya Afrika Kusini imeonekana kuingiliwa leo Ijumaa wakati nchi hiyo ikihesabu kura za uchaguzi mkuu ambapo chama tawala cha ANC kilionekana kupoteza wingi wake.