Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kipimo kwa Rais Samia.
Uchaguzi huu utatoa picha ya hali ya kisiasa nchini Tanzania, hasa kuhusu demokrasia, haki za kisiasa, na uhuru wa vyama vya upinzani.
Uchaguzi huu utatoa picha ya hali ya kisiasa nchini Tanzania, hasa kuhusu demokrasia, haki za kisiasa, na uhuru wa vyama vya upinzani.
Kwa mujibu wa taarifa ya TRC iliyotolewa leo idadi hiyo ni mara mbili ya waliosafiri na treni ya zamani ya (MGR), ambayo ilisafirisha jumla ya abiria 400,000 katika kipindi cha mwaka mmoja.
Derick Junior(36), Ofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), anayekabiliwa na mashtaka mawili ya kujeruhi katika Club ya 1245 iliyopo Masaki Dar es salaam, leo anatarajiwa kusomewa hoja za awali katika kesi inayomkabili.
Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema, kimeilalamikia mamlaka nchini humo kwamba wagombea wake wengi wamekataliwa “kwa njia isiyo ya haki” kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika wiki ijayo.
Mamlaka ya Uganda, ambayo ilisema kuwa zinachunguza taarifa za kupotea kwa Besigye, zimekuwa zikifanya ukandamizaji dhidi ya upinzani katika miezi ya hivi karibuni, kwa kuwakamata viongozi mashuhuri na kuwashtaki wanachama wa vyama vya upinzani.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Lawrence Nyasebwa Mafuru, amefariki dunia leo Novemba 9,2024 katika Hospitali ya Apollo nchini India.
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla, ametoa msisitizo kwa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kutenda haki kwa vyama vyote vilivyosimamisha wagombea katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa amewataka wagombea wote ambao hawajaridhishwa na uteuzi wa wagombea wa nafasi mbalimbali kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa waweke pingamizi ndani ya siku 2 kuanzia leo tarehe 08 – 09/11/2024.
Mkuu wa Taasisi ya Afya ya Umoja wa Afrika Jean Kaseya amesema maambukizi ya mpox yamepungua kidogo barani Afrika, ingawa bado janga hilo halijaisha.
Matokeo ya utafiti huo uliofanywa katika mikoa yote nchini, yanaonesha matumizi ya viuatilifu kwenye uzalishaji mboga za majani yanachangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la magonjwa yasiyoambukizwa kwa binadamu kama vile saratani, kisukari na matatizo ya uzazi.