Africa East Africa People Politics Tanzania

Uchunguzi wa CNN wafichua kaburi la pamoja la Watanzania waliouawa wakati wa mandamano.

Waathiriwa, wengi wao wakiwa hawana silaha, walipigwa risasi na polisi, miili yao ikitupwa kama takataka. Mwanamke mjamzito ambaye alijikuta katikati ya vurugu alifyatuliwa risasi mgongoni wakati akijaribu kukimbia. Daktari aliyewahudumia majeruhi aliripoti muundo wa kutisha wa majeraha ya risasi, hasa kichwani, tumboni, kifuani na kwenye miguu.