CCM yataka haki uchaguzi serikali za mitaa, yasema hawahitaji upendeleo
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla, ametoa msisitizo kwa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kutenda haki kwa vyama vyote vilivyosimamisha wagombea katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji.