Tanzania, Marekani kuongeza nguvu ya pamoja kukabiliana na ugonjwa wa Saratani
Tanzania na Marekani wamekubaliana kukabiliana na uhaba wa wataalamu, ukosefu wa miundombinu wezeshi, Vifaa Tiba hususani vya kutoa huduma za Mionzi, Takwimu, Tafiti pamoja na Ubunifu ili kuwezesha wananchi wa Afrika kupata huduma bora za Saratani bila kikwazo.