ACT Wazalendo yashinikiza uchunguzi wa Kimataifa dhidi ya mauaji ya waandamanaji
Taarifa hiyo ya ACT Wazalendo ambayo imetolewa leo Alhamisi Novemba 6, 2025, imeeleza kuwa matukio hayo si uvunjifu wa haki za binadamu tu bali pia mamlaka zimekosa utu kwa kutozingatia misingi ya utawala bora.