HRW:Kenya inapaswa kuchunguza miili iliyotupwa kwenye mgodi
Shirika la Haki za Binadamu la Human Rights Watch (HRW) limeiomba Serikali ya Kenya kumaliza uchunguzi kuhusu miili iliyoharibiwa iliyopatikana kwenye mgodi mwaka jana, na kushughulikia madai kwamba polisi walizuia juhudi za kuchukua miili hiyo.