Shahidi wa upande wa utetezi katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, John Heche, ameieleza Mahakama matukio mbalimbali ya mauaji, utekaji na kupotezwa kwa watu nchini, akitaja viongozi na wanachama wa vyama vya siasa waliopitia matukio hayo.

Akitoa ushahidi wake, Heche ametaja baadhi ya watu waliopotea au kutekwa akiwemo aliyekuwa Mjumbe wa Chadema, Ben Saanane, mwandishi wa habari Azory Gwanda, pamoja na watu wengine ambao alisema hadi sasa familia zao hazijui walipo.
Heche pia ameeleza kuhusu kesi mbalimbali za kisiasa zilizowakabili viongozi na wanachama wa Chadema, akiwemo Freeman Mbowe na yeye mwenyewe. Amesema Mbowe alikabiliwa na kesi ya ugaidi mwaka 2021 na kukaa gerezani kwa miezi minane kabla ya kuachiwa.
Kwa upande wake, Heche ameiambia Mahakama kuwa alikamatwa Oktoba 22, 2025 nje ya Mahakama Kuu kwa tuhuma za kuvuka mpaka kwenda Kenya bila kufuata taratibu, kabla ya baadaye kusomewa shtaka la ugaidi alipofikishwa kituo cha polisi Dodoma.
Akielezea kuhusu Lissu, Heche amesema alishawahi kukamatwa mara kadhaa katika kesi mbalimbali, ikiwemo mwaka 2014 huko Nyamongo ambako alikwenda kufuatia mauaji yaliyotokea mgodini. Amesema Lissu hakuwahi kutiwa hatiani katika kesi hizo, huku akieleza pia kuwa kesi nyingine za uchochezi zilizofunguliwa dhidi yake kati ya mwaka 2015 na 2020 ziliishia bila kuendelea.
Heche pia ameeleza mazingira ya shambulio la risasi dhidi ya Lissu lililotokea Septemba 7, 2017, akisema alishambuliwa mchana akiwa anaelekea nyumbani kwake Dodoma. Kwa mujibu wa ushahidi wake, hakuna mtu aliyewahi kukamatwa au kushtakiwa kwa tukio hilo.
Amesema baada ya shambulio hilo Lissu alisafirishwa kwenda Nairobi, Kenya kwa ajili ya matibabu na baadaye Ubelgiji. Heche ameeleza kuwa yeye mwenyewe alikwenda kumtembelea Lissu Nairobi mara kadhaa, huku akisema baadhi ya viongozi wa kitaifa waliwahi pia kumtembelea hospitalini.
Katika ushahidi wake, Heche amesema matibabu ya Lissu hayakulipiwa kwa utaratibu wa kawaida wa matibabu ya Mbunge, bali sehemu kubwa ya gharama iligharamiwa na Chadema, marafiki, wananchi pamoja na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), ambacho wakati huo Lissu alikuwa Rais wake.
Akirejea msimamo wa Chadema wa “No Reforms No Elections”, Heche amesema msimamo huo ulihusu mabadiliko ya Kikatiba na kisheria, ikiwemo namna Tume ya Uchaguzi inavyopatikana na kuwepo kwa Tume Huru ya Uchaguzi.
Amesema baada ya msimamo huo kufikiwa na Kamati Kuu ya Chadema, ulitangazwa hadharani na aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, Desemba 10, 2024. Baadaye Baraza Kuu la chama liliupokea na kuuunga mkono kabla ya kupelekwa kwenye Mkutano Mkuu wa chama uliofanyika Januari 21, 2025.
Heche amesema Mkutano Mkuu uliamua Kamati Kuu iandae mpango wa kuwafikia wadau mbalimbali, wakiwemo viongozi wa dini, wanachama na taasisi mbalimbali, ili kuwaeleza sababu za chama kufikia msimamo huo.
Ameongeza kuwa katika utekelezaji wa maazimio hayo, viongozi wa Chadema walikutana na wadau mbalimbali, akiwemo Ubalozi wa Marekani, Joseph Sinde Warioba, Joseph Butiku, Jukwaa la Wahariri, viongozi wa Kanisa Katoliki na LHRC, huku akisema Lissu ndiye aliyekuwa kiongozi na msemaji mkuu wa ujumbe huo
Hapa kuna maswali na majibu ya kilichoendela mahakamani (edited)
[2:25 PM]LISSU: Waeleze majaji kama kuna watu wa chadema walikamatwa wakati wa uchaguzi huo
Heche: Ndio viongozi wa chadema walikamatwa kuna mwenyekiti wa kinondoni kichama henry Kileo alikamatwa na mkurigenzi wa ulinzi wakati huo wilfred Rwakatare walishitkiwa wote kwa kesi kubwa za ugaidi henry alishitakiwa tabora mahakama baadae ikatupilia mbali na kuachiwa huru na Wilfred Rwakatare alishitakiwa hapa Dar na baadae mahakamma ikamuachia huru hiyo ni baada ya kuwa wamekaaa magerezani kwa muda mrefu
Lissu: Waeleze majaji kama kumekuwa na mauaji ya wananchi wengine wasio wanachama wa chadema
Heche: Waheshimiwa majaji kuna mauaji ambayo yana husisha wananchi wakati wa uchaguzi wa serikali za mtaa kuna maeneo ambayo yalitokea mauaji kama shinyanga tunduma yenyewe pia
Lissu: Waeleze majaji ufahamu wowote ulionao juu ya mauaji pemba na zanzibar
Heche: Waheshimiwa majaji wakati
Katuga: Hii aina ya uulizaji maswali waheshimiwa majaji ni kama mshitakiwa anatoa ushahidi
Jaji: sawa
Lissu: hilo swali sioni kamma linashida yoyote
Jaji: Nadhani upande wa jamuhuri wako sahihi ungemuuliza tu maeneo mengine kama yapo na sio kumuelekeza kwa kumtajia maeneo
Lissu: sawa
Lissu: Sasa waeleze majiji iwapo unakumbuka mauaji nje ya chadema maeneo mengine
Heche: Nakumbuka mauji ya mwaka jana wakati wa uchaguzi mkuu ambapo mamia ya watu waliuawa mauaji hayo yalifanywa na vyombo vya dola polisi mauaji makunwa yalifanyika Dar Mwanza mbeya Arusha Tarime Geita na maeneo mengine mengi
Lissu: Waeleze majaji juu ya utekwaji na upotezaji wa watu
Katuga: Huu ulizaji wa maswali nachoka kusimama waheshimiwa majaji haya maswali ni leading yana pendekeza majibu
Lissu: nimeshaondoka kwenye swala mauaji wakili wa serikali anasema lina sugest jibu Jibu gani kama kipo shahidi atasema kama hajui atasema sinui swala watu kupotezwa ni mjadala mzito nchi hiii na ni topic mpya kabisa na mlead vipi shahidi
Lissu: Vinginevyo nitaintroduce vip new topic waheshimiwa majaji
Jaji: tuna sisitiza tu tujilite kwenye taratibu za examination in chief tunaomba usiulize maswali yanayo suggest majibu
Lissu: naomba ni lirejee swali waheshimiwa majiji waambie majaji matukio mengine ya uonevu nje ya mauaji
Heche: matukio ya uonevu ni mengi ikiwemo watu kutekwa kupotezwa
Heche: katika hilo nitazungumza matukio kadhaa ninayo yafahamu
Heche: Ripoti ya TLS inasema kuna watu 718 waliotekwa na kupotezwa kati ya hao kuna viongozi wa chadema wanachama wa chadema viongizi wa vyma vingine vya siasa kama ccm ambao wameonesha msimamo wao wa wazi wa kupinga matendo ya serikali hii
Lissu: sinama hapo hapo shahidi
Jaji: ndio
Lissu: hujatuambia hiyo ripoti ya TLS ni ya mwaka gani tupe taarifa kamili
Heche: waheshimiwa majiji ripoti ya TLS mwaka 2026 imeeeleza matukio ya mwaka jana mwaka huu mwaka 2016/2017 ni ya muda mrefu waheshimiwa
Lissu: Tuanze na ya 2016/20217
Heche: 2016/2017 ni ya ben saaa nanene kutekwa na kupotea,azory gwanda alikuwa mwandishi kanguye aliyekuwa mwenyeki wa ccm huko kigoma
LISSU: aeleze Waheshimiwa majaji matukio yanutekaji unayoyafahamu
Heche: matuki ya kutekwa nankupotea watu mwaka 2016 ni kupotea kwa Ben Saanane, Azori Gwanda, Mwandishi wa Mwananchi, Kanguye aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri CCM Kigoma
LISSU: Waeleze Waheshimiwa majaji ufahamu wako hao watu walioatikna au vipi
Heche: mpaka leo familia ya Ben Saanane haijawahi kujua ndugu yao yuko wapi hivyo hivyo familia ya Azori Gwanda
LISSU: Waeleze Waheshimiwa majaji matukio mengine ya utekwaji kama yapo
Heche: Waheshimiwa majaji kuna matukio ya kutekwa kwa Balozi Humprey Polepole wa CCM, alikua mbunge, Balozi, DC, kuna matukio ya kutekwa Mdude Nyagari mwanachama wa Chadema mpaka sasa hajulikani alipo tangu 2024, Deusdedith Soka, Mwenyekiti wa Vijana wa Chadema kutoka Temeke, Jacob Mlaya alikua Katibu wa Chadema Temeke, Daniel Chonchori alipotea Tarime na alikua mjumbe wa mkutano Mkuu wa CCM Taifa, Sinda Geteba huyu alikua mgombea wa Udiwani wa CCM kata ya Sirali familia yake inadai alichukuliwa na RCO na mpaka leo hajarudi kuna Bhurure Tall alikua mwanachama wa Chadema, kuna Amani Manengero kutoka Mwanza alikua Mwenyekiti wa Vijana wa BAVICHA mkoa wa Mwanza. Kuna Nyangoko Kina huyu ni mwananchi alipotea Tarime, Sirali, kuna Deus Kipanya alikua kiongozi wa Sumbawanga wa Chadema, kuna Siza Kiheta huyu ni kutoka Tarime. Kwa sasa niseme hao tu kati ya watu wengi ambao wameweza kutekwa
LISSU: Jana wakati unatoa ushahidi ulielezea kesi uliyokuhusu wewe na Freeman Mbowe na wengine ambao walikua viongozi wa chama, naomba uwaeleze Waheshimiwa majaji ukiachia hiyo kesi ya mwaka 2018 Eleza kesi nyingine za kisiasa zinazokuhusu wewe zinazohusu viongozi wenzako wa Chama
Heche: Waheshimiwa majaji kuna kesi iliyomuhusu Mwenyekiti Mbowe kesi ya Ugaidi ilikua ni kesi ya mwaka 2021, baadae aliachiwa na tukaona picha yake ya kwanza Ikulu kwa Rais Samia Suluhu.
LISSU: Waeleze Waheshimiwa majaji hiyo kesi ya Ugaidi iluweka mwenyekiti gerezani kwa muda gani?
Heche: Kwa miezi minane, Waheshimiwa majaji hiyo kesi siku mwenyekiti anakamatwa Mwanza nilikamatwa nae pamoja na wanachama wengine baadhi ya viongozi wa dini tulipkuwa nao siku hiyo, Wazee nakumbuka tulikamatwa na Mzee Azaveri Lwaitama,
LISSU: Waeleze Waheshimiwa majaji huyu Azaveri Lwaitama ni nani
Heche: Dk. Azaveri Lwaitama kwa sasa ni Makamu Mwenyekiti wa bodi ya Wadhamini wa chama na mashauri wa Chama, tulikamatwa na mzee Masinde sasa ni Marehemu, John Pambalu alikua Mwenyekiti wa BAVICHA wakati huo, kwa sasa ni Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo Chadema, Baba Askofu Mwamakula, Mwenyekiti wa mkoa wa Njombe Rose Mayemba ambaye sasa ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema.
LISSU: Shahidi umesema mlikamatwa wote pamoja na Mwenyekiti halafu ukasema Mwenyekiti akafunguliwa kesi ya Ugaidi
Heche: Tulishikiliwa kwenye vituo mbalimbali vya polisi, wengine walikua Nyakato, Kirumba na mimi nilikuwa kwenye kituo kikuu cha Polisi Mwanza, tulikaa siku mbalimbali, mimi nilikaa siku tano pale na nikafanyiwa upekuzi na wengine walisafirishwa kwenye maeneo walikotokea kama Rose alipelekwa Njombe na Pambalu na Mzee Rwaitama walipelekwa Dar es salaam na baadae walifikishwa nyumbani kwao wakaachiwa.
LISSU: Shahidi endelea uwapo wa kesi zingine za aina hii
Heche: Mwaka jana mimi nilikamatwa hapa hapa nje ya Mahakama Kuu tarehe 22 Oktoba 2025, ilikua kwamba nimevuka mpaka kwenda Kenya bila kufuata taratibu ndio tuhuma niliyopewa nilipofikishwa hapo Central kwa bwana Mafwele.Kwa hiyo nilichukuliwa hapo nikaambiwa napelekwa sehemu nilipofanyia Kosa kwa maana ya Tarime. Tulianza Safari mpaka tulipofika Dodoma mida ya Usiku siku hiyo hiyo, nikapelekwa kituo cha Polisi Mtumba Dodoma,karibu na mji wa kiserikali nikawekwa kituo cha Polisi kwenye Selo ya peke yangu mpaka nilipokuja kutolewa tarehe 4 November kusafirishwa kurudishwa Dar es salaam. Waheshimiwa majaji nilipokua mule ndugu zangu hawakuruhusiwa kuja kuniona mpaka nilipogomea kula wala kunywa siku tatu ndipo ndugu yangu akaruhusiwa kuja kuniona
LISSU: Hiyo tarehe 4 November ulivyosafirishwa kuja Dar ulifikia wapi?
Heche: Nilipotolewa Dodoma nikafikishwa Dar es Salaam nikafikishwa kituo cha Polisi Oysterbay hapo siku hiyo niliwakuta kina bwana Wakili Nassoro Katuga, Wakili Job Mrema, Wakili Thawabu Issa na Wakili Cathbert Mbilinyi.
LISSU: Waeleze Waheshimiwa majaji kitu gani kilitokea?
Heche: Waheshimiwa majaji niliwakuta hawa Mawakili wa Serikali Wakuu siku hiyo kulikua na watu wengi sana pale kituoni, ambao walikua wamekamatwa wengine wamejeruhuwa niliambiwa wamekmatwa kwa sababu ya vurugu za uchaguzi waliwekwa kwenye selo zao mpaka kwenye Korido, hawa Mawakili walikua na bwana George Bagemu.
LISSU: Waeleze Waheshimiwa majaji kilitokea kitu gani ulipowakuta hawa mawakili wa serikali?
Heche: Nilipelekwa kwenye chumba ghorofa ya kwanza nikasomewa kwamba kosa la Ugaidi, kuchoma vituo vya Mwendokasi kuanzia Kimara hadi Ubungo kwamba mimi nilihusika kuchoma hivyo vituo
LISSU: Aliyekusomea shtaka la Ugaidi aikua nani?
Heche: Ni Askari simkumbuki
LISSU: Ikawaje baada ya kusomewa hayo mashtka ya Ugaidi?
Heche: Waheshimiwa Majaji sikua tayari kuandika maelezo yangu, walichukua tu majina yangu na mahali ninapoishi na baada ya hapo wakanipeleka Kituo cha Polisi Mburahati
LISSU: Ulikaa muda gani pale Oysterbay?
Heche: Nilikaa kwa masaa tu, kwanza nilipelekwa kituo flani hapo Kijitonyama tukaambiwa kimejaa kwa hiyo nikapelekwa Mburahati
LISSU: Ulipofika Mburahati kitu gani kilitokea?
Heche: Waheshimiwa majaji niliwekwa hapo kuanzia siku hiyo ya tarehe 4 November mpaka tarehe 10 November 2025
LISSU: Nini kilitokea baada kufikishwa Oysterbay?
Heche: Nilichukuliwa pale nikarudishwa kituo cha Polisi cha Oysterbay, nilikutana na Naibu Katibu Mkuu ndugu Aman Golugwa ambaye nae alikamatwa wakati anataka kusafiri, nilikutana na bwana Godbless Lema mjumbe wa Kamati Kuu, Boniface Jacob na Mjumbe wa Kamati Kuu wote hawa walikamatwa kwa hiyo tulikutana hapo. Tulipokutana hapo tulimkuta ZCO Mafwele ambaye alikuwepo pale akatuambia tudhaminiwe tuondoke na kesho yake tukaripoti November 12, 2025 tukaenda kuripoti.
Heche: Tulienda kuripoti hapo Central kwenye ofisi ya ZCO Mafwele akatuambia tuendelee na shughuli zetu.
LISSU: Hii tuhuma ya Ugaidi Waambie Waheshimiwa majaji iliishia wapi
Heche: Waheshimiwa majaji mimi sikukamarwa kwa tuhuma ya Ugaidi, nilikamatwa kwa tuhuma ya kuvuka mpaka wakati naenda kuhudhuria mazishi ya Raila Odinga, hii tuhuma ya Ugaidi nilipewa baada ya kufikishwa Polisi Dodoma. Na hizi tuhuma zimeisha tu
LISSU: Kama nilikusikia sawasawa ulisema kwenye ushahidi wako wa awali ulieleza kwamba tangu ulichguliwa kuwa Diwani 2008 mpaka leo miaka
LISSU: Yote hii kwa ufahamu wako kuna viongozi wa ngazi za juu za chama ambaye hakukamatwa kwa sababu zozote na kesi zikafutika futika tu kama hii
Heche: Waheshimiwa majaji sina kumbukumbu ya ambaye hajakamatwa
LISSU: Sasa Shahidi kwenye kesi hii mimi nimekamatwa kwa kadri ya taarifailiyoletwa Mahakamani waendesha mashtaka hii kesi ambayo unaitolea ushahidi leo. Waeleze Waheshimiwa majaji hii ni kesi yangu ya kwanza tangu unifahamu
Heche: Hii sio kesi ya kwanza kwa Mh. Tundu Lissu, nakumbuka alikamatwa mwaka 2014 maeneo ya Nyamongo, Nakumbuka pia alikamatwa mara kadhaa kwa kesi mbalimbali kama Uchochezi
LISSU: Kama unakumbuka nilipokamatwa, nilikamatwa kwa kesi gani?
Heche: Nakumbuka tukio lenyewe kuna watu waliuawa pale mgodini, Mh. Tundu Lissu alikuja pale kwa sababu kulikua nammsuguano kati ya ndugu na walioua kwa hiyo alikuja kama mtetezi wa wananchi wa Nyamongo na alikamatwa kwa kesi ya Uchochezi
LISSU: Na Waeleze Waheshimiwa majaji hicho kipindi nilikua na cheo gani ndani ya chama?
Heche: Waheshimiwa wakati huo Tundu Lissu alikua mbunge na Mkurugenzi wa Haki na Sheria wa Chama
LISSU: Waeleze Waheshimiwa majaji hiyo kesi ya Uchochezi iliishia wapi
Heche: Waheshimiwa Majaji kama ilivyo kwa kesi zingine iliisha tu
LISSU: Na Waeleze Waheshimiwa majaji hizo kesi zingine Za Uchochezi zilishaje
Heche: Waheshimiwa majaji kesi za Uchochezi ambazo Tundu Lissu alifunguliwa mwaka 2015 hadi 2020 na zenyewe ziliisha tu zingine inasemekana Serikali haikua na nia ya kuendelea nazo
LISSU: Sasa Shahidi naomba uwaeleze Waheshimiwa majaji kwa hizi kesi ambazo umesema nimekamatwa nazo, Waeleze Waheshimiwa majaji iwapo imetokea nimekamatwa nazo Waeleze kama ipo hata moja ambayo nimekutwa na hatia
Heche: Hakuna hata moja
LISSU: Na hivyo hivyo kwa viongozi na wanachama wa Chadema aliyefubguliwa kesi aliyekamatwa akakutwa na hatia akafungwa au kulip faini
Heche: Waheshimiwa Majaji Kama kwa ninavyofahamu ukiachia mbali ile tuliyokmatwa na kushtakiwa pale Kisutu sina kumbukumbu kwa waliotiwa hatiani hata mmoja
LISSU: Shahidi Waeleze Waheshimiwa majaji kuhusu kinga dhidi ya kukmatwa aliyonayo kiongozi yoyote au mwanachama yoyote?
Heche: Kwa ninavyofahamu hakuna kinga kwa kiongozi yoyote au mwanachama yoyote aliyonayo
LISSU: Waeleze Waheshimiwa majaji kwa unavyofahamu wewe iwapo kuna chama kingine chochote ambacho wanachama wake wamekamatwa, kushtakiwa, kuwekwa Mahabusu
Heche: Waheshimiwa majaji sina kumbukumbu kwa chama kingine ambacho viongozi wake wamewahi kushtakiwa
LISSU: Nilikuuliza kwamba Viongozi wa chadema wanakinga ya kukamatwa ukasema hapana, swali langu hii kamatakama kwa wanachama na viongozi wa chadema lengo lake hasa nini?
Heche: Lengo la kukamata wanachama na viongozi ni kuwatisha na kuwaktisha tamaa Nan kuwa rudisha nyuma kwenye misimamo mbalimbali ambayo chama imekubaliana
LISSU: Waeleze Waheshimiwa majaji uhalali wa maneno hayo yankukamata viongozi kwa lengo la kuwatisha kwa unavyofahamu
Heche: Hakuna uhalali wowote wa kufanya hayo, hakuna uhalali wa kisheria, wala uhalali wa kiutu, mimi jinachokiona ni kile alichokisema Katibu Mkuu wakati huo Bashiru Ally, kwamba “tutamia dola kuendelea kubaki kwenye dola” kwa hiyo haya matendo yanalenga kutumia dola kuendelea kubaki kwenye dola kwa CCM
LISSU: Shahidi umewaeleza Waheshimiwa majaji kwamba ulikua na mimi bungeni kuanzia 2015 kuelekeza 2020, Waeleze Waheshimiwa majaji kitu gani kilitokea tarehe 7 September 2017?
Heche: Yeye Alishambuliwa kwa risasi mchana wa tarehe 7 September 2017 akiwa anaenda kula chakula cha mchama katika makazi yake Dodoma
LISSU: Waeleze Waheshimiwa majaji siku hiyo ya tukio wewe ulikua wapi
Heche: Waheshimiwa majaji siku hiyo mimi nilikua Bungeni
LISSU: Waeleze Waheshimiwa majaji kitu gani kilitokea kabla ya hilo shambulio na baada ya shambulio unachokifahamu
Heche: Kabla ya hilo shambuli tulikua bungeni baadae mchana alienda nyumbani kwake ambapo alifatiliwa na gari mpaka kwenye eneo la nyumbani kwake eneo ambalo mimi nalifahamu kwa sababu niliwahi kwenda pale, kwenye hiyo sehemu viongozi kadhaa wa serikali na wabunge walikua wanakaaa kwenye eneo hilo.Mara zote ukiwa unaenda pale kunakua na askari ambapo anakuuliza unaenda wapi kulikua na kitabu cha kusaini, alifatiliwa na kushambuliwa pale nyumbani kwake, hao washambuliaji waliondoka ndani ya geti mpaka leo hakuna aliyewahi kushtakiwa wala kukamatwa kwa tukio hilo.
LISSU: Waeleze Waheshimiwa majaji baada ya hilo Shambulio kitu gani kilitokea
Heche: Baada ya hilo shambulio alisafirishwa kwenda Nairobi – Kenya kwenda kupata matibabu ambapo alitibiwa kwa muda mrefu na baadae Ubelgiji
LISSU: Sasa Waeleze Waheshimiwa majaji hizi taarifa za kutibiwa kwangu kwenda Ubelgiji wewe ulizijuaje
Heche: Waheshimiwa majaji nilizijua kwa sababu nilikua nae bungeni, hata hivyo nilimtembelea Nairobi hospital mara kadhaa, vilevile Spika wa Bunge wakati huo Job Ndugai sasa Marehemu alitutangazia bungeni.
LISSU: Waeleze Waheshimiwa majaji umesema umewahi kuwa mbunge Waeleze majaji utaratibu wa mbunge anapoumwa na kutibiwa nje unakuaje
Heche: Mbunge anapopata matatizo kama matatizo yake yanawezekana hapa nchini anatibiwa hapa kwa kutumia bima kubwa ya Wabunge, lakini kama ni nje ya nchi umepewa rufaa Ofisi ya Katibu wa Bunge inachukua jukumu la kulipia matibabu, eneo unalofikia pamoja na msaidizi wako unaekaa nae
LISSU: Sasa Waeleze Waheshimiwa majaji kama huo huo utaratibu ulitumika kwenye matibabu yangu
Heche: Utaratibu huo haukutumika kwa Mh. Tundu Lissu, hakulipiwa matibabu wala msaidizi wala eneo alikofikia akiwa anajiuguza.
LISSU: Waeleze Waheshimiwa majaji sasa kwa vile sikutibiwa kwa utaratibu wa kibunge nilitibiwaje?
Heche: Waheshimiwa majaji sehemu kubwa ya matibabu ilikua ni kutoka kwenye chama, chama kiliingia kwenye sehemu ya matibabu, michango ya marafiki, na TLS ambayo kwa wakati huo Lissu alikua rais wake nayo ilichangia marafiki hao ni pamoja na wananchi ambao walichangia wengi walienda mbali walichangia na damu pia
LISSU: Sasa Shahidi kwa vile kwenye ushahidi wako ulisema ulikua mbunge, Waeleze majaji kitu gani kilitokea kwenye ubunge wangu baada ya kuelekea kwenye matibabu?
Heche: Waheshimiwa majaji Mh. Tundu Lissu alivuliwa ubunge kwa sababu zilizoelezwa alikua ni mtoro bungeni
LISSU: Ilikua mwaka gani
Heche: Waheshimiwa majaji nakumbuka Mh. Tundu Lissu alikua bado yupo kwenye matibabu nje ya nchi Nakumbuka jimbo lake likaitishwa uchaguzi kuziba nafasi yake
LISSU: Shahidi Waeleze Waheshimiwa majaji ufahamu wako kuhusu aliyekuwa Makamu wa Rais wa Wakati huo Samia Suluhu kuja kunitembelea hospital Nairobi
Heche: Nakumbuka aliyekuwa Makamu wa Rais wa wakati huo Samia Suluhu alikwenda Nairobi kwa ziar Aya kiserikali lakini alikwenda kumuona Lissu hospital
LISSU: Kuhusu Tume ya Utumishi wa wabunge kuja kujitembelea hospitali
Heche: Waheshimiwa majaji hiyo sina kumbukumbu nayo
LISSU: Na Waeleze Waheshimiwa majaji ufahamu wako kuhusu aliyekuwa Rais Mstaafu marehemu mzee Ally Hassan Mwinyi na mke wake kuja kunitembele
Heche: Waheshimiwa majaji hilo nalikumbuka taarifa ilitoka kwenye vyombo vya habari kuhusu Rais Mwinyi na mkewe kwenda kumtembelea Mh. Lissu
LISSU: Na Waeleze Waheshimiwa majaji ufahamu wako kuhusu mawaziri wakuu wastaafu, Edward Lowassa, Sumaye na Warioba kuja kunitembelea hospital Nairobi.
Heche: Waheshimiwa majaji nina kumbukumbu ya Edward Lowassa kumtembelea mwenyekiti Nairobi, vilevile Fedrick Sumaye lakini sina kumbukumbu nzuri kuhusu mzee Warioba
LISSU: Waeleze Waheshimiwa majaji kuhusu Jaji Mkuu mstaafu Othman Chande kuja kunitembele Nairobi
Heche: Waheshimiwa majaji nina kumbukumbu hiyo ya Mh. Jaji Chande kumtembelea Lissu hospital
LISSU: Waeleze Waheshimiwa majaji ufahmu wako kuhusu balozi wa Tanzania nchini Kenya wakati huo Balozi Pindi Chana kuja kunitembelea hospital Nairobi
Heche: Waheshimiwa majaji ninayo kumbukumbu hiyo ya Mh. Pindi Chana kwenda kumtembelea Mh. LISSU alipokuwa Nairobi kwenye Matibabu
LISSU: Shahidi nimekuuliza maswali yote haya kwa sababu nataka niulize swali hili wewe umetumia muda gani kuja kuniona
Heche: Waheshimiwa majaji nimeenda mara kadhaa Nairobi siwezi kuwa na kumbukumbu ya muda gani nimetumia Nairobi lakini ni kama Mwezi, mara zingine wiki mbili lakini pia ni watu wengi wamekwenda kumtembelea.
LISSU: Sasa Shahidi turudi kwenye terhe 3 Aprili mwaka jana, kwenye ushahidi wako wa awali umeiambia Mahakama kwamba nia ya kuwaita watia nia kwenye huo mkutano ilikua ni kuwafahamisha na kuwaelimisha juu ya msimamo wa chama wa No Reforms No Elections, tuanzie hapo ni mabadiliko gani ambayo chama kilikua kinataka yafanyike ili iende kwenye uchaguzi
Heche: Waheshimiwa majaji ni mabadiliko ya Kikatiba na Kisheria. Sheria zinazoongoza uchaguzi, namna Tume inavyopatikana, KATIBA hasa kifungu cha 74 kinachounda hii Tume na kuwepo kwa Tume Huru inayotoa usawa kwa watu wote kwenye uchaguzi mkuu
LISSU: Shahidi kama nilikusikia ulisema kwamba msimamo huu wa mabadiliko hakina uchaguzi ulifikiwa kwenye kikao cha kamati kuu ya chama kilichofanyika tarehe 3 December 2024, sasa kipi kilifata baada ya msimamo huo kutangazwa na kamati kuu
Heche: Baada ya msimamo huo kufikiwa kwenye chama ulitangazwa hadharani na aliyekuwa Mwenyekiti wa chama wa wakati huo Freeman Mbowe kwamba baada ya yale yaliyojitokeza kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa wa 2024 mwezi November wagombea wetu kuenguliwa, hata wale walioshinda hawakutangazwa, kwa hiyo Mh. Mbowe akatangaza kwa niaba ya Kamati Kuu kwamba bila mabadiliko hakuna uchaguzi, kwamba uchaguzi hauwezekani kwenye nchi hii kwa njia hizi za kawaida
[2:28 PM]LISSU: Waeleze Waheshimiwa majaji hilo tamko la Mbowe lilikuwa la tarehe ngapi?
Heche: hilo tamko lilikua la tarehe 10 December 2024.
LISSU: Baada ya tamko la Mwenyekiti wa Chama wakati huo Mh. Mbowe kitu gani kilifata
Heche: Waheshimiwa majaji wakati huo pia tulikua tunaelekea kwenye uchaguzi wa ndani wa chama kwa hiyo vikao vilikuwepo vya kuandaa Baraza Kuu na Mkutano Mkuu ambapo Kamati Kuu ilikutana tarehe 19 Janauari 2025
LISSU: Waeleze Waheshimiwa majaji maamuzi gani yaliazimiwa kwenye huo mkutano wa Kamati Kuu.
Heche: Waheshimiwa majaji miongoni mwa mambo mengi yaliyopitishwa tamko la hiyo No Reforms No elections lilipitishwa kwenye baraza kuu la chama.
LISSU: Hicho kikao cha Baraza Kuu la Chama kilikua cha tarehe ngapi?
Heche: Tarehe 20, January 2025.
LISSU: Waeleze Waheshimiwa majaji kitu gani kilitokea kwenye hilo Baraza Kuu
Heche: Waheshimiwa Majaji, Baraza Kuu lilipokea ajenda hii na kuiunga mkono na baadae kuipeleka kwenye mkutano Mkuu wa Chama uliofanyika tarehe 21 January 2025
LISSU: Na kitu gani kilitokea kwenye mkutano mkuu?
Heche: Vilevile huu ulikua ni mkutano mkuu wa kiuchaguzi ambao ulimchagua Mh. Tundu Lissu kuwa Mwenyekiti wa Chama, Makamu Mwenyekiti wa Zanzibar Saidi Mzee na Makamu Mwenyekiti Bara John Heche
LISSU: Specifically agenda ya No Reforms No Elections Waeleze Waheshimiwa majaji nini kiliazimiwa
Heche: Mkutano mkuu uliazimia kwamba kamati kuu ya chama iandae mpango wa namna ya kuwafikia wadau mbalimbali, viongozi wa dini, wanachama kuwaelimisha kuwaambi kwanini chama kimefikia msimamo huu
LISSU: Na Waeleze Waheshimiwa majaji baada ya MkutanoMkuu kuamua hivyo kamati kuu ilifanya niniw
Heche: Kamati kuu ya Chama ilikutana kwenye retreat iliyofanyika Bagamoyo, na ikaazimia kwamba maazimio ya Mkutano Mkuu yatatekelezwa kwa maana kwamba viongozi wa Chama, Mwenyekiti wa Chama Mh. Tundu Lissu, Makamu wenye viti kutoka Bara na Zanzibar, Katibu Mkuu wa Chama John Mnyika, Manaibu Makatibu wakuu Bara na Zanzibar, viongozi wote wa chama katika kanda, tukutane na taasisi mbalimbali.Tukutane na viongozi wa kidini kwa maana ya dini zote, mabalozi, Wazee maarufu, NG’Os kueleza msimamo wetu huo kwamba waunge mkono huo msimamo ili mabadiliko yafanyike na uchaguzi ufanyike huru, haki na wa amani.
LISSU: Sasa Shahidi shtaka linalonikabili linasema kwamba nilisema maneno yenye maudhui ya kihaini na nikuachapisha kwenye mitandao ya kijamii. Naomba uwaeleze Waheshimiwa majaji kuhusu
Heche: Miongoni mwa watu ambao tulikutana nao ni Jukwaa l Wahariri tulizunhumza nao kama vile ambavyo tulizunhumza na viongozi wa dini NG’Os
LISSU: Katika wadau wote hao ambao tulikutana nao nataka uwaeleze Waheshimiwa majaji mikutano ambayo Mimi na wewe tulikuwepo
Heche: Tulitembelea Ubalozi wa Marekani, Tulimtembelea Mzee JosepySinde Warioba, Tulikutana na Mzee Joseph Butiku ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, tulizungumza na Jukwaa la Wahariri,tulimtembelea Rais wa Baraza la Maaskofu Wakatoliki, Askofu Kisa, tuliwatembelea LHRC
LISSU: Sasa kwa sababu tulikua pamoja nataka uwaeleze Waheshimiwa majaji nani alikua kiongozi na msemaji Mkuu wa ujumbe wetu
Heche: Kiongozi na Msemaji Mkuu alikua ni Mwenyekiti Tundu Lissu.
Kesi inaendelea