Samia:Vurugu za Oktoba 29, zimeishushia hadhi Tanzania Kimataifa
Rais Samia Suluhu Hassan amesema sifa ya Tanzania kama kisiwa cha amani imeanza kuporomoka kutokana na matukio ya vurugu, uchochezi na matumizi ya dini katika siasa, akisisitiza kuwa vitendo hivyo vinadhoofisha misingi iliyoiweka nchi hiyo kwenye heshima ya kimataifa kwa miongo mingi.