Wahukumiwa miaka saba jela kwa jaribio la kumteka mfanyabiashara Tarimo
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni, Kinondoni, jijini Dar es Salaam, imewahukumu vijana wanne kifungo cha miaka saba jela kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kujaribu kumteka mfanyabiashara Deogratus Tarimo.