Chadema yaikata Tume ya Rais Samia, yashinikiza uchunguzi wa Kimataifa
Makamu Mwenyekiti wa Chadema, John Heche, akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Novemba 19, 2025, amesema Rais Samia hana mamlaka ya kimaadili wala kisiasa kuunda chombo cha kuchunguza kile chama hicho kinachokitaja kuwa ni uhalifu uliotekelezwa na Serikali yake dhidi ya raia waliokuwa wakidai haki zao za kidemokrasia.