Lissu: Hati ya mashtaka haina msingi wa kisheria
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, Lissu anatuhumiwa kwamba mnamo Aprili 3 alikusudia “kuchochea wananchi kuzuia uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.” Hata hivyo, mwanasiasa huyo mashuhuri anasema kosa hilo haliingii kwenye wigo wa makosa ya uhaini kwa mujibu wa sheria za Tanzania.